STEVEN WAMBURA:Msanii wa muziki wa Injili aliyeamua kuwekeza kwenye studio
MUZIKI wa Injili umekuwa ukikua siku hadi siku na kuzidi kuibua vipaji miongoni mwa jamii hasa vijana.
Steven Wambura
Steven Wambura ni mmoja wa vijana hao ambapo sasa ni msanii wa muziki wa Injili, huku muziki wake ukiwa ni wa bolingo na rumba.Kipaji cha Wambura kilianza kuonekana mwaka 1987 alipokuwa akiimba kwaya katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Bethel Kijenge mkoani Arusha.
“Wakati huo nilikuwa bado nakisoma na masomo yangu yalikuwa magumu, nakumbuka nilipigwa na wazazi na wakati mwingine kulazwa njaa kutokana na kujihusisha na masuala ya muziki,” anasema.
Wambura anasema kuwa kipindi hicho wazazi wake
walikuwa hawapendi ajishughulishe na muziki na kwamba mara zote walikuwa
wakimsisitizia asome.
“Siwezi kuwalaumu, inawezekana walikuwa wanaogopa kwa sababu kulikuwa na dhana kuwa muziki wa Tanzania haulipi, lakini sasa muziki ndiyo unaendesha maisha yangu,”anasema.
Anaeleza kwamba baada ya kumaliza kidato cha nne
mwaka 1993, aliendelea kuimba kwaya hadi mwaka 1994, alipoamua kuanzisha
bendi yake iliyoitwa Chipukizi, ambayo alidumu nayo hadi mwaka 1997.
“Bendi haikudumu sana na mwaka 1998 niliajiriwa kwenye duka moja la dawa mkoani Arusha. Mwaka uliofuata niliamua kwenda nje kutafuta maisha,” anasimulia.
Anasema kuwa mwaka 2003 alirudi nchini na
kuendelea na shughuli za uimbaji, ambapo aliamua kutoka kwenye mfumo wa
kwaya na kuwa muimbaji binafsi.
Wambura anaeleza kuwa wakati akiendelea na
shughuli za uimbaji binafsi, aliamua kuokoka mwaka 2005 na Mungu
kumjalia kutoa albamu mbili ambazo ni Bwana ndiye bwana na Roho wa
bwana.
Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hizo ni Bwana ndiye bwana, Bwana ndiye mchungaji wangu, Ita jina la yesu, Upendo, Nilitembea tembea, Bwana u sehemu yangu, Usilie tena na Nataka nikujue.
“Albamu zote hizi zilifanya vizuri sokoni na kunivutia niendelee na muziki,”anasema.
Hata hivyo, anasema kuwa licha ya mafanikio aliyoyapata katika uimbaji, alikuwa na ndoto ya kumiliki studio yake binafsi, ambayo itajikita katika uandaaji wa muziki, vipindi maalumu pamoja na mahubiri.
“Msukumo wa kuanzisha studio hii na kuwekeza kiasi
kikubwa cha fedha lengo lake siyo kufanya biashara, bali kuujenga
ufalme wa Mungu na kuwasaidia wengine kutimiza ndoto zao,”anasema
Wambura.
Wambura anadokeza kuwa licha ya kuwa na maono ya kupata kazi nzuri wakati huo, lakini alikuwa akikwamishwa na kasoro mbalimbali.
“Nilipoyazingatia hayo, niliona ni vyema kujitahidi kwa kadri ya uwezo na maarifa aliyonipa Mungu kutengeneza studio yenye ubora kama zile tunazofuata nje ya nchi,”anasema.
Licha ya kurekodi, studio hiyo pia watakuwa wakitoa ushauri na mafunzo kwa wafunga vyombo, pamoja na kwa waimbaji wa makanisani mbalimbali.
“Pamoja na kurekodi na kuandaa vipindi, Niko Ambaye Niko’ imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa mafunzo kwa waimbaji makini wenye wito na vipaji, ili wahudumu katika mikutano ya ndani na nje,”anasema Wambura.
Licha ya mafanikio aliyoyapata, Wambura anasema kuwa amekutaka na vikwazo vingi hasa kutokana na aina ya uimbaji wake wa ‘Bolingo na Rumba’ kwa sababu watu wengi walitaka aimbe taratibu huku akijinadi kuwa hawezi kubadili aina hiyo.
Elimu na mahusiano
Wambura alimaliza kidato cha nne mwaka 1992 katika Shule ya Sekondari Kimandulu iliyoko mkoani Arusha. Kuhusu mahusiano, msanii huyo alisema kuwa anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
Anaongeza: “Mimi ni muimbaji wa nyimbo za Injili na nimehangaika
maeneo mbalimbali kurekodi na wakati mwingine sikufanikiwa kupata kazi
kwa ubora niliokusudia.”
Anafafanua kuwa studio hiyo aliyoipa jina la ‘Niko
Ambaye Niko’ imegharimu Sh37 milioni na kwamba ni miongoni mwa studio
za kisasa katika ukanda wa Afrika Mashariki, akieleza kuwa suala la
ubora ndilo lililomsukuma kuanzisha studio.
Wambura anadokeza kuwa licha ya kuwa na maono ya kupata kazi nzuri wakati huo, lakini alikuwa akikwamishwa na kasoro mbalimbali.
Anabainisha kuwa suala hilo limesababisha baadhi
ya kwaya na waimbaji binafsi kusafiri hadi nje ya nchi kwa ajili ya
kurekodi na kutumia gharama kubwa.
“Nilipoyazingatia hayo, niliona ni vyema kujitahidi kwa kadri ya uwezo na maarifa aliyonipa Mungu kutengeneza studio yenye ubora kama zile tunazofuata nje ya nchi,”anasema.
Licha ya kurekodi, studio hiyo pia watakuwa wakitoa ushauri na mafunzo kwa wafunga vyombo, pamoja na kwa waimbaji wa makanisani mbalimbali.
“Pamoja na kurekodi na kuandaa vipindi, Niko Ambaye Niko’ imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa mafunzo kwa waimbaji makini wenye wito na vipaji, ili wahudumu katika mikutano ya ndani na nje,”anasema Wambura.
Licha ya mafanikio aliyoyapata, Wambura anasema kuwa amekutaka na vikwazo vingi hasa kutokana na aina ya uimbaji wake wa ‘Bolingo na Rumba’ kwa sababu watu wengi walitaka aimbe taratibu huku akijinadi kuwa hawezi kubadili aina hiyo.
Hata hivyo, anasema kuwa licha ya kuwa na studio,
bado ataendelea kuimba na kwamba atajikita kupiga muziki wa ‘live’
pamoja na bendi.
Elimu na mahusiano
Wambura alimaliza kidato cha nne mwaka 1992 katika Shule ya Sekondari Kimandulu iliyoko mkoani Arusha. Kuhusu mahusiano, msanii huyo alisema kuwa anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
Anasema kuwa matarajio yake ya baadaye ni kuwa na
kituo cha redio ili kurahisisha kazi ya kupeleka habari njema kwa kila
mtu na kwamba mchakato wa kupata masafa unaendelea.

Post a Comment