NIGERIA MABINGWA WAPYA WA SOKA AFRICA
NIGERIA mabingwa wapya Afrika 2013,yailaza Burkina Faso 1-0 katika mchezo wa fainali nchini Afrika Kusini.
Ni
shangwe na vigelegele katika miji mbalimbali nchini Nigeria baada ya
timu yao ya The Super Eagles, kuibuka mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa
ya Afrika.
Mbio
za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika zilizoanza tarehe 19 Januari
zimehitimishwa, Jumapili, tarehe 10 Februari kwa Nigeria kuibuka bingwa
wa fainali za mwaka 2013 barani Afrika.
Bao
la mchezaji Sunday Mba alilofunga katika dakika ya 40 ya kipindi cha
kwanza cha mchezo mjini Johannesburg, ndilo lililowahakikishia The Super
Eagles, Nigeria kuwa mabingwa wapya.
Mchezo
huo ulianza kwa kasi, timu zote mbili zikishambuliana kwa zamu. Hata
hivyo Nigeria ndiyo walionekana kutawala zaidi mpambano huo na kukosa
magoli kadha ambayo yangeipa ushindi mnono Nigeria.
Vijana
hao wa Super Eagles, wamekuwa wakiimarika kila hatua ya mashindano
hayo, hasa baada ya kufuzu kutoka katika makundi. Ni katika hatua ya
makundi ambapo mabingwa watetezi, Zambia walitolewa na kuachia kombe
hilo kufukuziwa na timu nane zilizoingia robo fainali, na hatimaye timu
mbili zilizotinga fainali, Nigeria na Burkina Faso.
Emmanuel
Emenike aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo na kupata kikombe,
huku Moses Victor akiwa mchezaji bora wa mechi kati ya Nigeria na
Burkina Faso.
Mechi
hiyo ya fainali ilihudhuriwa na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akiwa
mgeni rasmi, akiambatana na rais wa Fifa Sepp Blatter na rais wa CAF,
Issa Hayatou.
The Super Eagles pia waliahidiwa zawadi kem kem, zikiwemo fedha taslim kwa kocha na wachezaji, hata kabla ya kutwaa ubingwa.
Hii
ni zawadi kubwa kwa kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi ambaye mwaka
1994, wakati Nigeria ilipotwaa ubingwa wa Afrika, alikuwa nahodha wa
timu hiyo katika fainali zilifanyika nchini Tunisia.
Pia Nigeria ilitwaa ubingwa mwaka 1980, wakati fainali hizo zilipoandaliwa nchini Nigeria.
Super
Eagles kama ilivyo kwa timu nyingine barani Afrika, itakuwa ikijiandaa
kikamilifu kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia zitakazofanyika
nchini Brazil mwaka 2014.
Via saluti5

Post a Comment