Kuzaa kabla ya ndoa si dhambi, lakini unaweza kujipanga
KAMA
ilivyo ada tumekutana tena kwenye kona yetu ya Mapenzi na Uhusiano
kujuzana mawili matatu kuhusiana na maisha yetu ya kila siku. Yangu hali
namshukuru Mungu sijambo kiasi, sijui ninyi wasomaji wangu.
Leo
nataka kuzungumzia matatizo wanayokutana nayo wanawake wengi
wanaozalishwa na kuachwa bila huduma yoyote. Wengi wamekuwa wakipoteza
dira ya maisha, hasa wanafunzi ambao wanapobeba ujauzito, husababisha
kukatisha masomo na kuwa mwanzo wa kuyumba kimaisha.
Wapo ambao
hukutana na mwanaume kwenye safari au kwenye mahafari yoyote na kujikuta
wakishiriki tendo la ndoa bila kinga wakati hawajuani historia, wakati
mwingine mwanamke anakuwa katika siku za hatari za kubeba ujauzito.
Inawezekana kabisa ulikuwa kwenye starehe ya muda mfupi lakini baada ya
kuachana unajikuta umeshika ujauzito.
Mnapoachana na mwenzako ambaye hamkupanga kuzaa zaidi ya starehe, hata ukimuona au ukimpigia simu anaweza akakutosa kwa vile hakujiandaa kuzaa na wewe.
Ingawa kwa upande mwingine inashangaza! Mtu anapokutana na msichana bila kutumia kinga anategemea nini, kama siyo kupata gonjwa la zinaa au
kumuachia ujauzito?

Huwa sikubaliani na mtu aliyekutana kimwili na mwanamke bila kinga, kuruka futi mia anapoelezwa amempa ujauzito mwenzake.
Napenda kuwatahadharidha wasichana wengi ambao ndiyo wapo kwenye janga la maambukizi au kubeba ujauzito kabla ya wakati, kwamba wanatakiwa wawe na uamuzi sahihi, hasa wa kukataa kitu ambacho wanaona kina madhara kwao.
Wengi wamejikuta wakiingia katika mapenzi kwa tamaa ya vitu kama fedha na simu ambazo hutumiwa na wanaume wakwale wanaoamini ile ndiyo njia ya kuwanasa wasichana ambao wamejiingiza katika dunia ya kisasa ya mtandao wa mawasiliano.

Niliishaelezea huko nyuma madhara ya simu kwa
wasichana wadogo, hasa wanafunzi wanaotumia muda mwingi kuchati na
marafiki kwenye BBM, Facebook, Twitter. Vitu hivi vimekuwa ndiyo chanzo
cha wasichana wengi kujiingiza katika uhusiano na kusababisha kupata
ujauzito na mwisho wake kuacha masomo na kuwa chanzo cha kupoteza dira
ya maisha.
Tatizo kama hili halipo kwa wanafunzi au wasichana wadogo tu, bali limewakumba wanawake wengi, kiasi cha kufikia hatua ya kuongezeka kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Tatizo kama hili halipo kwa wanafunzi au wasichana wadogo tu, bali limewakumba wanawake wengi, kiasi cha kufikia hatua ya kuongezeka kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Hili si
tatizo la kujaa tu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, bali
kuongezeka kwa wanawake wanaoishi maisha ya kubahatisha na mwisho wake
kuangukia kwenye ukahaba kwa vile hana kazi, ana mtoto mdogo na aliyempa
mimba hakubaliani naye kwa vile hawakupanga au alikuwa ni mume wa mtu.
Hali hii inaweza kuepukika kama mtu atajitambua kwa kujipangia maisha yake na kujua muda gani unamfaa kupata mtoto na muda gani si sahihi. Hata kwa wanafunzi nao wanatakiwa kutambua muda wa masomo ni wa masomo, mapenzi baadaye.

Umeshaanza mapenzi, utajilindaje?
Kama una uhusiano na mtu ambaye hamna malengo naye, usikubali kubeba mimba. Mtoto mara nyingi hutafutwa kwenye ndoa kwa vile wanandoa wana malengo ya kuishi kwa muda mrefu. Kwa vile una rafiki na ni lazima mkutane kimwili, basi tumieni kondomu. Si kwa kujikinga tu na Ukimwi, bali kujijengea misingi imara ya maisha.
Kwa kujitambua, wote wenye malengo katika maisha yao wajue kuzaa kwa bahati mbaya si dhambi. Lakini lazima watambue kubeba mimba bila kupanga si fasheni bali kujiingiza kwenye matatizo yasiyo ya lazima.
Tumia tarehe za mzunguko wa hedhi ili kujikinga na mimba zisizotegemewa, kama hujui tumia kondomu, hivi vyote ukivifuata vitakufanya uwe salama.
Kwa hayo machache tukutane wiki ijayo.
Post a Comment