AFCON 2013: SOUTH AFRICA 2 vs ANGOLA 0
Timu ya Afrika ya Kusini leo imeichapa Angola kwa jumla ya magoli 2 - 0
katika mchezo wa kundi A uliocheza katika uwanja wa Nelson Mandela
Durban Afrika ya Kusini.
Magoli hayo yamefungwa na Siyabonga Sangweni na Lehlohonolo Majoro.
Wachezaji wa Afrika ya Kusini wakishangilia baada ya kupata goli

Vijana hao wa Bafana Bafana walianza mechi hiyo vyema kuliko walivyocheza katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Cape Verde.
Katika kipindi cha kwanza ilifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Angola.
Kunako dakika ya kumi na tano Afrika nusura ifunge bao lakini msaidizi wa refa wa mechi hiyo aliinua kijibendera kuashiria kuwa alikuwa ameotea.
Dakika mbili baadaye Bafana Bafana ilifanya shambulio lingine na mkwaju wa Siyabonga Sangwen ulikosa gola kwa ncha.
Kunako dakika ya 30 Siyabonga Sangweni akaifungia Afrika Kusini bao lake la kwanza.
Bao hilo lilionekana uwapa nguvu wachezaji wa Afrika Kusini ambao waliendeleza mashambulio yao dhidi ya Angola.
Afrika Kusini ingelifunga magoli zaidi katika kipindi hicho lakini wachezaji wake kadhaa walikosa umakini wakati wa kumalizia kwa kupoteza pasi nzuri walizopewa na wakati mwingine kupiga mpira ovyo.
Hata hivyo juhudi zao hazikufanikiwa na kufikia wakati wa mapunziko Afrika Kusini ilikuwa ikiongoza kwa bao moja kwa bila.
Kabla ya mechi hiyo kocha wa Afrika Kusini alikuwa amewashutumu wachezaji wake kwa kukosi umakini wakati wa mechi muhimu na inaonekana kuwa mazungumzo yake na wachezaji wake imeonekana kuzaa matunda.
Kipindi cha pili kilianza huku Angola ikiwa na wachezaji kumi pekee baada ya refa wa mechi hiyo kuanza mpira kabla ya kuruhusu mabadiliko katika kikosi cha Angola.
Kinyume na iliyokuwa katika kipindi cha kwanza wachezaji wa Angola walianza kuonana na kufanya mashambulio kadhaa katika lango la Afrika Kusini.
Lakini, licha ya juhudi hizo, Afrika Kusini ilipata bao lake la pili kunako dakika ya 61 kupitia kwa mchezaji wake wa ziada Lehlohonolo Majoro, ambaye alikuwa ameingia uwanjani dakika mbili tu kabla ya kufunga bao hilo.
Wa vuvuzela mpo hapo!! Mashabiki wa Africa kusinisiku ya jana

Post a Comment