Obrey Chirwa Ndiyo Kila Kitu Yanga, Ata Akikosa Penalti 20!
BENCHI la Ufundi la Yanga likiongozwa na Mzambia, George Lwandamina limeshindwa kujizuia na kutamka kuwa, Obrey Chirwa ndiyo kila kitu pale Jangwani.
Kauli hiyo, imetolewa na kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’ huku akisisitiza kwamba kila kitu kitakwenda sawa.
Chirwa, hadi sasa tayari amefunga mabao 10 huku akishika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji huku Mganda, Emmanuel Okwi akiongoza akipachika 13.
Akizungumza Nsajigwa alisema; “Chirwa ni mchezaji muhimu na tegemeo la Yanga, kama unavyoona washambuliaji wote ni majeruhi, hivyo uwepo wake unaimarisha kikosi chetu kinachotetea taji letu la ubingwa.”
“Chirwa ni aina ya wachezaji tunaowahitaji katika timu wanaoipambania timu yao ili iweze kupata matokeo mazuri ya ushindi, kiukweli nimpongeze kwa hilo,”alisema Nsajigwa mchezaji wa zamani wa Yanga, Prisons na Moro United.
Mastraika wawili tegemeo kwa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe ni majeruhi huku hali ya Ibrahim Ajibu na yenyewe ikiwa si nzuri kwa asilimia zote.

Post a Comment