- Uwanja wa ndege wa O. R. Tambo Afrika Kusini.
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetoa tahadhari kwa Watanzania wanaoingia
Afrika Kusini kupitia Uwanja wa
Ndege wa Oliver Tambo, ambapo kuna magenge ya watu wanaoendesha vitendo vya kuvamia na kunyang'anya wageni kutoka nchi mbalimbali mali zao zikiwemo
fedha taslim, mabegi, nguo , pete za ndoa na vitu vingine vya thamani.
Uporaji
huu hutokea hasa kwa wasafiri wanaoingia nchini humo kuanzia saa 12
jioni na kuendelea. Mbinu zinazotumika kuwatapeli na kuwaibia wageni
zipo chini katika barua iliyotolewa na wizara hiyo.
Post a Comment