Mastaa wa Kike Bongo Wadaiwa Kujiuza Kutokana na hali ngumu
DAR ES SALAAM: Kumekuwa na skendo nzito kwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo kudaiwa kujiuza kutokana na hali ngumu ya maisha lakini mara zote wakiulizwa huwa wanakataa hivyo kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kujipa kazi ya kutafuta ukweli wa ishu hiyo.
Ukiacha mastaa wakubwa waliowahi kuingia kwenye mtego wa skendo hiyo kwa OFM, tukio bichi ni la mwigizaji wa sinema za Kibongo, Husna Idd ‘Sajent’ ambaye juzikati alijikuta akiingia mkenge baada ya kachero wa OFM kujifanya mtayarishaji wa sinema kutoka mkoani Geita ambapo mrembo huyo alikubali ‘mambo’ kwa dau la shilingi laki nane (800,000) za Kitanzania.
Mwigizaji huyo, bila kujua yupo mtegoni alijikuta akiwa tayari kutoa penzi kwa kigogo huyo wa OFM kwa makubaliano ya kumaliza kwanza shughuli za ‘shutingi’ walizokubaliana awali.
MAMBO YALIANZA HIVI;
Aprili 16, mwaka huu, dawati la habari la gazeti hili lilipokea taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa Bongo ambacho kilidai kuwa, baadhi ya mastaa wa sinema za Kibongo wanaendelea na tabia hiyo hivyo ni vyema jambo hilo likafanyiwa kazi ili kuwaumbua. Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, wengi wao wamekuwa wapiga mizinga kwa wanaume ambao wanatokea kuzoeana nao kwa muda mfupi huku wakijirahisisha au kuwa tayari kutoa penzi kwa dau nono. “Naomba kuwapeni ishu ninyi OFM.
Naombeni muwaumbue hawa mastaa wa Bongo Muvi ambao wana tabia za kuombaomba pesa kwa wanaume na kujiuza maana wanakera sana. “Imefika hatua hadi ukiona simu yake anakupigia, unaanza kuogopa na kufikiria mizinga,” alitonya mnyetishaji huyo na kuwaachia OFM ‘shughuli’ yao.
MIPANGO YASUKWA
Kwa kuwa madai hayo yalihusisha mastaa wengi, OFM iliwaweka wote kwenye ‘tajeti’ lakini katika wote, Sajent aliingia kwa haraka zaidi, kilichofanyika ni kuandaliwa kachero mmoja wa OFM na kuwekwa katika namna ya kuonekana kama ‘bosi kubwa’ wa kampuni fulani. Baada ya hapo, Sajent alivutiwa simu na kachero huyo na kumwomba waonane kuzungumza mambo ya kikazi lakini mazungumzo hayo ndiyo yaliyozaa habari hii kwani
yaliishia katika makubaliano ya kukutana nyumbani kwa Sajent, Sinza-Meeda jijini Dar.
SAJENT MIKONO MWA OFM Aprili 19, mwaka huu, majira ya saa 9:00 alasiri, OFM walizingira nyumbani kwa Sajent huku wakiwa na zana za kazi kama vile kamera za video na picha mnato bila kusahau vinasa sauti. Kachero wa OFM aliyejifanya bosi kutoka Geita anayejishughulisha pia na uandaji wa filamu, hatimaye akaonana na Sajent na kuanza mazungumzo wakiwa wameketi kwenye kibaraza cha nyumba anayoishi mwanamama huyo.
Makubaliano ya awali juu ya kazi ambayo kachero wa OFM alijifanya kutaka kuifanya na Sajent walikubaliana ambapo staa huyo alitaka alipwe shilingi milioni moja na laki mbili (1, 200,000) za Kitanzania kwa ajili ya filamu ambayo Sajent atacheza kama mhusika mkuu. Baada ya makubaliano hayo, OFM aliondoka kwa ahadi ya kuendelea kuwasiliana huku wakingoja siku ya kulipana malipo ya awali (advance) kabla ya kuingia kwenye shutingi.
SAJENT MTEGONI
Apirili 21, mwaka huu, majira ya saa tatu na dakika kumi asubuhi, Sajent alimtumia Kachero wa OFM ujumbe mfupi uliosomeka: “Mambo vipi bosi, nyumbani kwangu umeme umekwisha, naomba nitumie pesa kidogo ninunue umeme.
” Baada ya kutuma ujumbe huo, OFM akataka kuthibitisha zaidi ndipo akamwendea hewani ambapo mambo yalikuwa hivi; Bosi: Nimeona ujumbe wako, lakini kuna jambo moja nataka tukubaliane Sajent, ukweli ni kwamba nimekuwa ni mwanaume ninayekutaka kwa muda mrefu, nitakuongezea shilingi laki nane kwenye ile shilingi milioni moja na laki mbili ili iwe shilingi milioni mbili kama utanikubali niwe mpenzi wako kwa muda mfupi tu.
Sajent: Dah! Sawa, lakini unaonaje tukimaliza kwanza kazi kisha mambo ya mapenzi yawe baada ya kumaliza hii project?
Bosi: Siyo tatizo, lakini kwanza nihakikishie kama uko tayari kwa hilo.
Sajent: Niko tayari ila baada ya kazi kumalizika.
Bosi: Kweli?
Sajent: Kabisa!
HITIMISHO Baada ya makubaliano hayo, OFM alimuahidi Sajent kumpatia kiasi hicho cha fedha hivyo. Sajent anaingia kwenye listi ya mastaa waliowahi kuingia mtego wa kujiuza wa OFM wakiwemo, Jacqueline Pentzel, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’, Baby Madaha, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ na wengineo
Post a Comment