Linah, Kijijini Kwenu Mitandao Ipo? Anachofanya si Utamaduni wa Mtanzania
Kuna vitu vingine inakuwa vigumu kuviacha vipite bila kuvizungumzia, hasa vinapofanywa na watu ambao unaamini kabisa kuwa wao walipaswa kuwa mstari wa mbele kukemea.
Juzikati nimeona picha katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Mwanamuziki, Estelina Sanga maarufu kama Linah, akilinadi tumbo lake ambalo lina ujauzito. Inawezekana kama baadhi ya watu wanavyojaribu kumtetea, kuwa hiyo ni furaha ya mimba yake ya kwanza.
Mara kadhaa tumezungumza kuhusu umuhimu wa watu maarufu kuwa mabalozi wazuri wa kulinda na kutetea maadili ya Mtanzania, lakini bahati mbaya wao ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kutuangusha.
Huu si utamaduni wa Mtanzania, ni tabia za watu wa Magharibi na Marekani, ambao kukaa utupu mbele ya watoto au watu wazima wenzao ni jambo la kawaida.
Kibantu, kitovu cha mwanamke ni sehemu nyeti, ambayo haipaswi kuonekana ovyo. Sasa inapotokea mtoto wa kike akapiga picha yenye kuonyesha kitovu na akaibandika katika sehemu ambayo kila mtu ataiona, hiyo ni fedheha kwake na familia yake.
Kusema kuwa hiyo ni furaha ya mimba yake ya kwanza siyo kweli, kwanza hakuna uhakika kuwa hii ni mimba yake ya kwanza, huenda ni ya pili, tatu au nne. Huu ni ulimbukeni tu ambao kukaa kimya ni kubariki ujinga katika jamii yetu.
Sina uhakika kama Linah alitaka kuwaonyesha ujauzito wake watu wa kijijini kwao, maana huenda huko waliko hawaamini kama anakaribia kuwa mama. Lakini hata kama ni hivyo, kwani ni lazima picha iwe ya utupu ndiyo waamini?
Ninachokiona, Linah alikuwa anataka kutuonyesha mchoro wake aliouchora tumboni, ambao hakuna jinsi ambavyo angeweza kutuonyesha kama siyo kusingizia picha ya ujauzito. Na huu ndiyo ulimbukeni wa mabinti wengi waliobarikiwa kupata umaarufu hapa Bongo.
Wanajitahidi kufanya kila wawezalo ili watu waone utupu wao, ndiyo maana hata ukitazama video za kazi zao, wamejaa uzungu pori. Halafu watu kama hawa, wakipata matatizo kwenye ujauzito una-weza kum-kuta akisin-gizia watu uchawi, wakati mchawi ni yeye mwenyewe!
Post a Comment