ad

ad

Wema, Jike Shupa Kimenuka...Kisa kipo hapa


Ule ushosti wa staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu na muuza sura kwenye video za wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ unadaiwa kuvunjika na sasa kila mmoja yupo na mambo yake,

Chanzo makini kililieleza kuwa wawili hao kwa sasa hawana ushosti tena kutokana na watu kuzungumza mengi kuhusu Jike Shupa huku wakimkataza Wema kuendelea kuwa na ukaribu naye kwa kile wanachodai kwamba tabia zake siyo nzuri.

“Watu wamekuwa wakimpigia Wema kelele za kuacha ushosti na Jike Shupa kwa sababu ya tabia zake maana kila mara amekuwa akionekana akifanya vitendo vya ajabu hadharani kama kunyonyana ndimi na wanaume tofautitofauti, kubadili wapenzi kila kukicha huku akihusishwa pia na usagaji,” kilisema chanzo hicho.

Katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram hivi karibuni mdau mmoja aliweka picha ya Jike Shupa wakiwa pamoja na Wema na kusema ni mashosti ambapo Wema alijibu na kumkana Jike Shupa hadharani kwamba siyo rafiki yake. “Wema kafuta urafiki na James Delicious sasa hivi kaunda urafiki na msagaji Jike Shupa, dada una marafiki wabovu hawaendani na hadhi yako, angalia wewe…,” aliandika mdau huyo.

Baada ya kuandika hayo Wema alijibu hapohapo na kuandika “Excuse me, sina ushoga na huyo mtu…kujuana na mtu na kuongea naye ndiyo kawa shoga…please…”

Mara baada ya posti hiyo kuwekwa, wadau wengi mitandaoni walishambuliana kwa lugha kali ambapo  wengine walisimama  upande wa Wema, wengine walimtetea Jike Shupa. Kutokana na majibizano hayo na Wema kumkana live, paparazi wetu alimtafuta Jike Shupa ambaye alikiri kuona alivyokanwa lakini bado mwanadada huyo akadai atabaki kuwa ndugu yake hawawezi kuacha kuwasiliana kamwe.

“Kwanza mimi siyo msagaji jamani na sijawahi kufanya hivyo, kuhusu Wema kunikana sioni shida na amefanya hivyo kwa sababu watu wamekuwa wakimuandama sana kwa sababu ya ushoga wetu,” alisema Jike Shupa.

Alipotafutwa Wema ili aweze kufunguka sababu za kumkana shosti yake, simu yake haikupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi,  hakujibu.

No comments

Powered by Blogger.