Breaking NewsR: ais Magufuli Ateua Mkuu mpya wa Majeshi Tanzania anaechukua nafasi ya Mwamunyange
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli,
amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni
Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.
Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Major Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
Major Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni
Jenerali.
Luteni Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Tanzania.
Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.
Post a Comment