PICHA YA MKUDE, MSUVA WAKIWA PAMOJA NDANI YA GARI YAZUA GUMZO MTANDAONI

Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, gumzo ni wachezaji wawili, Simon Msuva wa Yanga na Jonas Mkude wa Simba.
Wawili
hao wanaonekana wakiwa katika gari moja, wengi mtandaoni wanaichukulia
kama sehemu kuwa huenda Mkude ndiyo njiani kujiunga na Yanga kwa kuwa
suala lake la usajili na Simba linaonekana kuwa na shida.
Kiuhalisia,
Mkude na Msuva ni marafiki wa karibu kwa kuwa wote wako katika umri
mmoja ‘aga mate’ na wamecheza pamoja sehemu mbalimbali kwa maana ya
upinzani lakini wakiwa pamoja mfano timu za vijana na taifa.
Ingawa watu hawajaeleza au kujua kwamba picha hiyo ni ya hivi karibuni au ya kitambo.
Wanaojadili
mitandaoni, wengi wanaamini Msuva anaweza kumshawishi kutua Yanga. Wako
wanaomkaribisha na wengine wakionyesha hawana shida naye Yanga.
Kwa
mashabiki wengi wa Simba, wengi wanapuuza kwa kusema “aende zake”, wako
wanaonya kwamba awaangalie akina Ramadhani Singano na wengine na
wengine wanamshauri kuwa makini wakiamini Yanga huua vipaji vya
wachezaji wengi wanaotokea Simba. MJADALA UNAENDELEA.
Post a Comment