MKUU WA MKOA WA MOROGORO AIPOKEA FURSA
Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Mh. Kebwe S Kebwe, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Darasa la Fursa
mapema leo kwenye ukumbi wa Midland Msamvu Morogoro.
Mkurugenzi wa Clouds
Media Group Ruge Mutahaba akiwapa mbinu baadhi ya wakazi wa Morogoro za
kujikwamua kwa kutumia Fursa zilizopo Mkoani hapo.
Mkuu wa Chuo cha
Mlimani Professional Hassani Ngoma akiwaeleza namana alivyofanikiwa kimaisha
wakazi wa Morogoro.
Msanii wa Muziki wa
Hip Hop Bongo Nikki wa Pili akiongea jambo kwa wakzi wa Morogoro juu ya kutumia
fursa za mkoa huo ili kufanikiwa kimaisha.
Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Steven Kebwe (katikati), akiongea jambo na Ruge baada ya kuwasili
ukumbini hapo.
Baadhi ya wafuatiliaji
wa semina hiyo wakibadilishana mawazo.
Sehemu ya wakazi wa
Borogoro waliojitokeza kujifunza kwenye darasa la kifursa mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe akiagana na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.
MKUU wa mkoa wa
Morogoro Mh. Kebwe S. Kebwe, mapema leo alipata muda wa kuwakaribisha na
kuwapokea wazungumzaji wa Darasa la Fursa ambalo limekuwa likifanyika kila mkoa
ambapo tamasha la Fiesta linafanyika.
Kebwe aliipokea timu
nzima ya fursa ndani ya ukumbi wa Midland uliyopo maeneo ya Msamvu mjini Mrogo,
ambapo alienda kulifungua darasa hilo na kuwashuhudias baadhi ya wakazi wa mkoa
wake walivyojitokeza kusikiliza na kuonyeshwa namna ya kutumia rasilimali za
mkoa huko katika kujikwamua.
Akizungumza mara baada
ya kuingia katika ukumbi huo Mh, Kebwe alisema kuwa amefurahishwa sana na timu
ya Fursa na hasa Clouds Media Group kwa kuwafikishia tamasha la Fiesta ambalo
kwake anaamini lina mchango mkubwa sana kwa wananchi wake hasa katika kuongeza
kipato na kuwafanya wananchi wake kwa aslilimia kubwa kutumia fursa hiyo
kujifunza mambo mengi.
“Nimpongeze sana
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba kwa kutambua umuhimu wetu na
kuamua kutuletea tamasha la Fiesta likiwa limeambatana na darasa la Fursa, natambua
watu wengi hawaelewi umuhimu wa darasa hili ila kwangu mimi ninajua wananchi
wangu watajifunza nini leo kupitia Fursa maana kama ilivyo kauli mbiu yake ni
kweli kabisa watu wataongeza thamani kwa kupitia mafunzo haya,” alisema Mh. Kebwe.
Post a Comment