FIESTA MORO YAMVISHA SUTI STAMINA, PICHA SI ZA KUKOSA ZIPO HAPA ZOTE
Stori:
Mwandishi Wetu Morogoro
SHOO ya Fiesta
2016,juzikati ilimvisha suti msanii wa muziki wa kufoka foka kutoka mkoani hapo
Stamina, kiasi cha kuwafanya baadhi ya wasanii wenzake kumtania kwa kumwambia
kuwa atakua amepania kuwakomoa.
Tukio hilo
lilitokea ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini hapo ambapo Msanii huyo alipanda
jukwaani hapo akiwa ni msanii wa pili baada ya ratiba ya wasanii wakubwa kuanza
ambapo alitanguliwa na Chrisian Bella.
Stamina
alifanya makamuzi ya nguvu na kujikuta muda wote akipata shangwe nyingi kutoka
kwa ndungu zake hao huku akifuatiwa na Vanessa Mdee ambaye naye alifanya
makamuzi yake huku akifuatiwa Mr Blue ambaye alikuwa akifanya makamuzi yake ya
kufunga shoo takribani siku zote tangu tamasha hilo lilipoanza kurindi kwa mara
ya kwanza jijini Mwanza ambapo lilizinduliwa.
Ratiba ya shoo
iliendelea kuteka hisia za mashabiki kwani baada ya Mr Blue alipanda mtoto wa
mama Saidi Chege aliyefanya makamuzi ya nguvu huku akimpisha Sholo Mwamba,
ambaye alitumia jukwaa hilo kuutambulisha muziki wa Singeli kisha kumuachia
jukwaa mkongwe wa burudani Mr Msifa Dully Skes ambaye naye aligonga ngoma zake
kisha kumuachia uwanja huo mtoto wa Morogoro Belle9.
Makamuzi
hayakuishia hapo kwani ukiangalia ratiba na wingi wa wasanii wote waliopanda
ungeweza kusema hata nusu ya waliyokuwa bado hawakuifikia kwani baada ya Belle
9 ndiyo kwanza ratiba mpya ilifunguliwa na Hamadai kwa kuruhusu muziki wa Bendi
ambapo alipanda na wimbo wa Ipo siku yangu tu wa God luck Gobert.
Bendi ilizidi
kupamba moto kwani Hamadai aliimba sambamba na Nandy huku Maua Sama akisimama
kidete kuitikia baadhi ya kolasi za wimbo nyimbo hizo hadi pale ngoma ilipo
pamba moto na watatu hao kuamua kushuka na kumuachia jukwaa alitawale, Baraka
Da Prince.
Usiku huo
ulikuwa wa aina yake hasa ukilinganisha na wasanii walivykuwa wakipishana
ambapo baada ya Baraka Da Prince kutoka alichukua kipaza sauti hicho Ben Pol,
ambaye naye alifanya vilivyo hadi pale Jux alipopanda na kuimba wimbo wao wa
Nakuchana wa pamoja kisha kushuka wote na kumuachia jukwaa Darasa.
Hapo ndiyo
muziki wa kufoka foka ulipochukua nafasi kwa mara nyingine tena kwana baada ya
Darasa alipanda mwamba wa kanda ya ziwa Faridi Kubanda ‘Fid-Q, kisha kukitimua
vilivyo hadi pale naye alipoamua kumuachia jukwaa hilo Manfongo.
Singeli nayo
iliwanogesha mashabiki wa burudani kwa kiasi kwani baada ya Manfongo alipanda
Snura ambaye naye alitumia jukwaa hilo kutikisa chura wake kiasi cha
kuwapagawisha mashabiki wa Morogoro na kuwaachia kijiti cha burudani hizo crow
ya Weusi ambao kwa pamoja walifunga burudani za Fiesta mjini hapo.
Wikiendi hii
Fiesta inatarajiwa kuendelea katika mikoa ya Tanga na Moshi ambapo ratiba
inasema kwamba siku ya Ijumaa ya Septemba 23 makamuzi ya Fiesta yataendelea
ndani ya Uwanja wa Mkwakwani Tanga kisha jumapili ya Septemba 25 katika uwanja
wa Ushirika mjini Moshi.
Wasanii watakao
tumbuiza kwenye shoo hizo ni pamoja na Weusi,Shetta,Mr Blue,Manfongo,Ben
Pol,Christian Bella,Maua Sama,Nay wa Mitego,Snura,Madee, Navykenzo, Darasa,Dogo
Janja,Jambo Squad, Barnaba, Makomando,Nedy Music, Sholo Mwamba na Hamadai.
Post a Comment