SERENA HAKAMATIKI KWENYE TENISI, ABEBA TAJI LA WIMBELDON NA KUMFIKIA GWIJI, BEYONCE, JAY Z WASHUHUDIA
Serena
Williams sasa hakamatiki katika mchezo wa tenisi baada ya kumtwanga
Mjerumani, Angelique Kerber na kubeba taji la 22 la Wimbeldon.
Serena kutoka Marekani, amepata ushindi unaomfanya kufikia rekodi iliyokuwa inashikiliwa na gwiji la tenisi Steffi Graf.
Kerber alimshinda Serena na kubeba Australian Open Januari, mwaka huh na kuwashangaza wengi.
Lakini
leo, Serena alionekana yuko katika kiwango kizuri licha ya kuwa na
miaka 34 na kufanikiwa kumgaragaza Mjerumani huyo kwa seti za 7-5 na 6-3
kwa ulaini kabisa.
Rapa maarufu, Jay Z na kimwana wake, Beyonce walikuwa jukwaani wakishuhudia.
Post a Comment