HATIMAYE SIMBA, MAYANJA MAMBO SAAFIIII....ATAENDELEA NA KAZI YAKE KAMA KAWA
Baada
ya kuibuka kwa sitofahamu ya muda mrefu kuhusiana na ajira ya Kocha
Jackson Mayanja kama ataendelea na Simba msimu ujao au la, hatimaye
mambo sasa yameanza kukaa sawa na muda si mrefu kocha huyo anaweza
kutangazwa kama msaidizi wa kocha mkuu, Joseph Omog kuelekea msimu ujao.
Awali
kulikuwa na kikwazo cha kusubiri tamko la Omog kama angependa kuendelea
naye au la ambapo hilo likapita na kuibuka jipya la yeye kuamua kati ya
ofa ya Simba au Kagera Sugar walikomwita akasaini mkataba wa kuwa kocha
mkuu.
Hata
hivyo, baada ya mazungumzo ya takriban siku mbili na uongozi wa Simba
wakawa wamemalizana kila kitu kasoro kwenye ishu ya mshahara lakini hilo
nalo sasa limekwisha na Mayanja ameanza kuhudhuria katika mazoezi ya
timu hiyo akisubiri kumwaga wino saa yoyote kutoka sasa.
Makubaliano
yaliyofikiwa na pande hizo mbili ni kumpa kandarasi ya miaka miwili
kocha huyo itakayomalizika mwaka 2018, ikiwa sawa na muda anaomaliza
mkataba Omog klabuni hapo.
Mayanja alipotafutwa ili kupata ufafanuzi kuhusiana na hilo ambapo alisema:
“Kwa
kifupi niseme tu mazungumzo yanaendelea vizuri, nimeona kuna nafasi
nzuri ya kuendelea kubaki Simba ukizingatia niliishi na uongozi na
mashabiki vizuri tu msimu uliopita ni vizuri ikieleweka hivyo kwa sasa.”
Alipotafutwa
Katibu wa Simba, Patrick Kahemele kuzungumzia hilo, hakupatikana.
Alipopigiwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans
Poppe simu yake haikuwa hewani, upande wa Rais wa Simba, Evans Aveva
yeye simu yake iliita bila ya kupokelewa.
Post a Comment