AZAM FC WAFUNGUKA SUALA LA KIPRE TCHETCHE KWENDA YANGA
Uongozi wa Azam FC umesisitiza suala la mshambuliaji wake Kipre Tchetche kusajiliwa na Yanga ni hadithi za mtaani.
Msemaji
wa Azam FC, Jaffar Iddi ‘Mbunifu’ amesema imekuwa kila msimu kuna
taarifa za kusajiliwa kwa Tchetche na Yanga. Lakini hakuna hata kiongozi
ambaye amewahi kuwasiliana na uongozi wa klabu hiyo.
“Sijui
nani anazusha haya mambo, Kipre ni mchezaji wa Azam FC. Hakuna timu
inayoweza kumsajili pembeni zaidi ya kufuata utaratibu.
“Kama
ni kumhitaji, utaratibu unajulikana. Nisingependa kuzungumza mambo
mengi kwa kuwa hatujawahi kusikia kiongozi wa Yanga mfano mwenyekiti au
katibu akuzungumzia hili. Lakini kila mara linaibuka, sijui ni sehemu ya
propaganda au kampeni za uchaguzi.
“Kwa kifupi, Kipre ni mchezaji halali wa Azam FC, full stop,” alisema Jaffar akionyesha kujiamini.
Kumekuwa na tetesi ambazo hazina uhakika kuhusiana na suala hilo ambazo zimesambaa mitandaoni na baadhi wamekuwa wakiziamini.
Post a Comment