ad

ad

Rufani ya Wasira yawekewa pingamizi

 Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini, Rosemary Ibrahim, amesema kesi ya rufani iliyowekwa na wapigakura wa Jimbo la Bunda Mjini dhidi ya mbunge wa jimbo hilo, Esther Bulaya, ataitolea uamuzi Machi 14, mwaka huu, baada ya mawakili wa wajibu maombi kuwasilisha pingamizi.
 


Jaji Ibrahim alisema baada ya wajibu maombi kuwasilisha pingamizi la kutaka kutupiliwa mbali rufaa hiyo, mahakama hiyo itatoa maamuzi yake Jumatatu ijayo Machi 14, mwaka huu.

Naye Mwanasheria wa Serikali, Paschal Marugu, aliieleza mahakama hiyo kuwa katika maombi hayo kumeonekana kuna kiapo kilichoapwa na Wakili Mutalemwa, lakini aliyethibitisha ni Denis Kahangwa ambaye hakuapa kiapo hicho ikiwa ni kinyume cha sheria.

"Kwa mujibu wa kanuni, kiapo kinatakiwa kuapwa na mtu aliyethibitisha na sio vinginevyo, hivyo kiapo hicho kimeonyesha kuwa ni batili na kupoteza maana, naiomba mahakama yako iyatupilie mbali maombi hayo kwa mujibu wa sheria," alisema Marugu.

Kwa upande wa waleta maombi ambao waliwakilishwa na wakili Constantini Mutalemwa, waliiomba mahakama hiyo kutenda haki katika kusikiliza ombi hilo kufuatia pingamizi lililoletwa na wajibu maombi, huku akisimamia katika baadhi ya vifungu vya sheria vinavyoeleza kama kuna sehemu imeonyesha kuna makosa ya kiuchapishaji, hivyo mahakama haina haja yakumnyima haki mleta maombi kutokana na dosari hizo.

Wapigakura wanne, walipeleka pingamizi Mahakama Kuu kwa lengo la ‘kumtetea mbunge’ aliyeshindwa, Stephen Wasira, wakidai mbunge aliyeshinda, Bulaya, alicheza ‘mchezo mchafu’ na kutangazwa mshindi.

CHANZO: NIPASHE

No comments

Powered by Blogger.