Lulu amezua minong’ono Bongo Muvi hadi kufikia hatua ya kutengwa
Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ameendelea kuzua minong’ono kutokana na kitendo cha kutoshiriki kwenye mikusanyiko ya wasanii wenzake hadi kufikia hatua ya kutengwa.
Hali
hiyo ya sintofahamu ilijidhirisha Jumanne iliyopita kwenye hafla ya
kumpongeza Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa
na wasanii wa Bongo Muvi chini ya uratibu wake, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ katika Hoteli ya Rodizio iliyopo Masaki, jijini Dar.
“Jamani!
Mbona Lulu hajifunzi kutokana na makosa? Juzi alipokuwa akirudi na tuzo
kutoka Nigeria, hatukwenda kumpokea kutokana na yeye kutokupenda
kujumuika na wasanii wenzake, angalia sasa, hata leo hajaja kama kawaida
yake.
“Nilidhani
atabadilika kumbe wapi. Anapaswa kubadilika sababu sioni cha kumzuia,
mbona akialikwa kwenye pati za rafiki zake huwa anakwenda lakini sehemu
kama hizi haji? Kilichotokea Airport ni funzo tosha, Mungu alimpa na
akiendelea hivi siku atakumbana na majanga mazito atakosa wa kumsaidia,”
alisikika mmoja wa wasanii waliokuwepo katika hafla hiyo.
Mara baada ya kupokea malalamiko hayo, mwandishi wetu alimtafuta Lulu na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka hivi:
“Sababu zangu kutohudhuria katika hafla zao wao wenyewe wanazijua na wakizijua wao inatosha siyo lazima nikwambie na wewe (mwandishi). Elewa tu hivyo.”
“Sababu zangu kutohudhuria katika hafla zao wao wenyewe wanazijua na wakizijua wao inatosha siyo lazima nikwambie na wewe (mwandishi). Elewa tu hivyo.”
Post a Comment