Kerr amkingia kifua Isihaka kwa utovu wa nidhamu
Nahodha msaidizi wa Simba, Hassan Isihaka.
BAADA ya nahodha msaidizi wa Simba, Hassan Isihaka kusimamishwa na uongozi wa klabu hiyo kwa kile kilichoelezwa ni utovu wa nidhamu, aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Muingereza, Dylan Kerr amesema haamini kama kweli mchezaji huyo amefanya kosa kama hilo.
Mbali na kusimamishwa huko, pia Kamati ya Utendaji ya Simba imeagiza Isihaka kulipwa nusu mshahara kwa kipindi chote cha adhabu yake hiyo.
“Isihaka ni mchezaji mzuri na mwenye nidhamu, hivyo sidhani kama kweli anaweza kufanya kitendo kama hicho kwani kwa muda niliokaa naye sikuwahi kuona akiwa mtovu wa nidhamu.
“Lakini Mayanja anapaswa kuelewa kwamba amepata bahati sana kurithi mikoba yangu pale Simba, hawezi kukaa vizuri na wachezaji kwani hata alipokuwa Coastal wachezaji walikuwa wakimlalamikia, sidhani kama atakuwa na maisha marefu pale,” alisema Kerr.
Post a Comment