
Profesa Ibrahim Lipumba akiongea jambo mahakama ya Kisutu.
Profesa
Ibrahim Lipumba na wafuasi 30 wa CUF leo wameachiwa huru na Mahakama ya
Kisutu Dar kwa kuandamana na kukaidi amri ya polisi.Kesi hiyo imefutwa rasmi leo baada ya DPP kuieleza mahakama kuwa hana nia tena ya kuendelea na kesi hiyo.
Mara baada ya kuwasilisha hati hiyo mahamani, Cyprian Mkeha, hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, ameamuru kufutwa kwa kesi hiyo na kuamuru kumwachia huru.
Prof. Lipumba alikuwa akitetewa mahakamani na Peter Kibatala. Wakili huyo aliieleza mahakama kutokuwa na pingamizi na hatua hiyo.
Prof. Lipumba na wafuasi 30 wa chama hicho walishitakiwa kwa madai ya mkusanyiko usio halali, tarehe 22 na 27 Januari mwaka huu, wilayani Temeke.
Mkusanyiko huo ulikuwa maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya mauaji wa 15 waliouawa Unguja na Pemba, Januari 26 na 27 mwaka 2001.
Mongoni mwa wafuasi hao, ni pamoja na Shabani Ngurangwa (56), Shabani Tano au Kasakwa (29), Shabani Polomo (40), Juma Mattar (54), Mohammed Kirungi (40), Athumani Ngumwai (40), Shaweji Mohamed Mketo (39) na Abdul Juma Kambaya (40).
Hata hivyo, tarehe 26 Februari mwaka huu wafuasi hao 30 wa CUF waliokuwa wakikabiliwa na kesi hiyo, walifutiwa mashitaka na DPP.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Garson Msigwa, Prof. Lipumba alikutana na Magufuli kwa lengo la kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa rais.
Post a Comment