SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI
MSHAMBULIAJI Ibrahim Hajibu wa jana usiku ametokea benchi na kuifungia Simba SC mabao matatu katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa ya Jang’ombe Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Simba SC imeshinda 4-0 na hiyo inakua hat trick ya pili katika mashindano haya baada ya awali Simon Msuva wa Yanga kuwafunga hao hao Taifa mabao matatu peke yake katika ushindi wa 4-0 pia, mchezo wa Kundi A.
Simba SC sasa itasubiri mshindi wa mchezo kati ya mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda na Polisi ya hapa, ikutane naye katika Nusu Fainali Jumamosi.
Hajibu aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Awadh Juma, alifunga mabao hayo dakika za 46, 63 na 75, kabla ya Shaaban Kisiga ‘Malone’ aliyetokea benchi kufunga la nne dakika ya 80.
Post a Comment