ad

ad

TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 13



ILIPOISHIA
“Yule ndiye mke wa MJ?”
“Mke! Malaya tu.”
“Ina maana si mpenzi wake wa siku zote?”
“MJ ana mpenzi mmoja? Kila kukicha anabadili wanawake kama nguo. Huyu sijui mtoto wa kigogo alikuwa nje ya nchi nasikia kaidanganya familia yake anakuja kesho ili ale raha na MJ jana na leo kisha kesho anakwenda kwao.”
“Amefika lini?”
“Jana usiku.”
“Saa ngapi?”
Songa nayo....
“Kama saa tano au sita hivi sina kumbukumbu vizuri.”
“Wakati anakuja MJ alikuwa wapi?”
“Sijui si unajua anapenda starehe sana, alinipigia simu tu nimpokee na baadaye alikuja mwenyewe.”
“Kwenye saa ngapi?”
“Bebi maswali yote ya nini mbona unauliza kama mpenzi wako?”
“Samahani bebi nimeuliza tu.”
“Achana naye tufanye yetu, ukimfuatilia MJ atakupasua kichwa, sijui mwanamke gani jijini hajampitia.”
“Mbona mimi hajanipitia?” Lily alijishaua.
“Bahati yako uko na mimi bila hivyo sasa hivi ungekuwa umeliwa na kupigwa chini.”
“Kwa hiyo ndiyo tabia yake?”
“Lily hebu tuachane na mambo ya MJ,” Shuku alisema huku akifungua mlango wa gari na kumuingiza Lily kisha alirudi upande wake na kuingia kwenye gari na kuelekea kwenye msosi.
Lily moyo ulimuuma baada ya kujua MJ alimtelekeza hotelini kwa ajili ya yule msichana. Moyoni aliapa kumshikisha adabu tena kupitia kwa Shuku mulemule ndani.
Lily baada ya kutoka kwa Shuku alipanga kulirudisha penzi lake upya kwa mpenzi wake baada ya kuona MJ alimfanyia kitendo cha kumdhalilisha. Alipoorudi nyumbani alimueleza yote dada yake aliyofanyiwa na MJ.
“Mdogo wangu dunia ya leo hakuna bwana wa mmoja, wee kula sehemu yako isiyokuhusu waacheni wenzako.”
“Dada unauma hawezi kunitelekeza hotelini na kwenda kwa mwanamke mwingine.” Lily alisema kwa uchungu.
“Kwa hiyo ulitaka kufanyaje?”
“Nimeona heri nirudiane na Shuku.”
“Kwani mliachana?”
“Hatukuachana bali nilipenda nimtulikie bwana mmoja Shuku nilikuwa namtema kiana.”
“Una muda gani ulikuwa hujaonana na Shuku?’
“Muda kidogo nilikuwa nimpiga kalenda mpaka akashtuka, dada leo mbona nilikuwa ndo aachwa!”
“Na nani?”
“Na Shuku.”
“Kwa sababu gani?”
“Si sababu ya kumrusharusha, penzi alilonipa leo lilikuwa la mwisho,,ha..halafu sa..aa..sa!”
“Nini tena?” dada Lily alishtuka.
“Dada japokuwa Shuku mbahiri lakini ni mwanaume wa shoka, akikushika kakushika. Alichonipa leo kama angeniacha ningeingia uchizi.”
“Kakupa penzi gani tena lililokuchanganya mdogo wangu?”
“Hata siwezi kulielezea ila sijawahi kupewa penzi tamu kama lile.”
“Sasa mdogo wangu kwa vile Shuku hajui lolote juu ya uhusiano wako na MJ, wewe mpe penzi kama kawaida ila hakikisha hupitishi siku mbili lazima umpe.”
“Nitafanya hivyo, sasa hivi mpenzi yote kwa Shuku kuchuna kwa MJ.”
“Umeona eeh, mdogo wangu hayo ndiyo mambo usiwe na hasira za mkizi bure.”
“Habari ndiyo hiyo.”
Simu ya Lily iliita alipoangalia alikuta ni MJ amepiga, alitulia bila kupokea kitu kilichomshtua dada yake na kuhoji.
“Vipi nani, mbona hupokei?”
“MJ.”
“Sasa mbona hupokei?”
“Yaani kanitoka moyoni ile mbaya.”
“Hebu pokea kumbuka ndiye anayekupa jeuri mjini.”
“Dada nitazungumza naye nini?”
“Msikilize.”
Lily alipokea simu, alikuzungumza:
“Haloo.”
“Haloo Lily mpenzi samahani sana.”
“Samahani ya nini MJ?”
“Kwa yote niliyokufanyia nakuahidi kukufanyia mambo makubwa naomba unisamehe sana pia sitaki tuyakumbuke yaliyopita, ila naomba jioni ya leo tuonane samahani sana mpenzi wangu,” MJ alijitetea.
“Sawa nimekusamehe ila suala la kuonana nitakujibu baadaye.”
“Basi usichelewe kunijulisha mpenzi.”
“Poa,” Lily alijibu huku akikata simu.
”Vipi anasemaje?” dada Lily aliuliza.
“Eti anaomba msamaha.”
“Nimefurahi kusikia umemsamehe mdogo wangu ukitaka kula na kipofu usimshike mkono.”
“Lakini dada nimemsamehe kwa ajili yako kitendo alichonitenda kiliniumiza sana.”
“Kikuumize vipi wakati kuna wasichana wenzako nawatumika bure lakini wewe una gari na nyumba inakuja.”
“Eti anataka leo tuonane.”
“Kwa hiyo?”
“Aah! Mi siendi, Shuku anaweza kunitafuta itakuwaje nami sitaki kumuudhi tena?”
“Kwani mlikubaliana leo muonane?’
“Tumeagana tu, anaweza kunitafuta ili kuona niliyomuomba msamaha nayatekeleza.”
“Sasa fanya hivi mkubalie MJ, Shuku akikupigia mwambie mi mgonjwa.”
“Jamani akija na kunikosa itakuwaje?”
“Fanya hivi mwambie MJ akupitie saa mbili ili tujue kama Shuku atakutafuta tujue tufanye nini.”
“Ngoja basi nimpigie kumujua tukutane wapi.”
“Mpigie.”
Baada ya kupiga simu ilipokewa upande wa pili.
“Haloo.”
“Haloo.”
“Niambie mpenzi?”
“Kwa hiyo?”
“Nakusikiliza wewe.”
“Leo wapi?”
“Pa jana.”
“Saa ngapi?”
“Saa mbili usiku.”
“Utanifuata?”
“Noo bebi njoo tu na usafiri wako.”
“Poa.”
Baada ya kukata simu alimgeukia dada yake.
“Amesema kama jana.”
“Nenda mdogo wangu kijua ndicho hiki ndo wakati wa kuuanika.”
“Nimekuelewa dada, naomba tu Shuku asinitafute.”
Kwa vile alikuwa amechoka baada ya kuoga Lily alipanda kitandani kulala.
****
Majira ya saa mbili usiku kama kawaida Lily alipaki gari lake maeneo ya Sea Cliff hoteli. Alimpigia simu MJ na kumueleza kila kitu alikwisha lipia alimueleza akachukue ufunguo mapokezi ili atangulie chumbani.
Lily alifanya kama alivyoelekezwa kwa kuchukua funguo na kuingia chumbani kumsubiri MJ kwa kuagiziwa kila kitu alichokitaka kutumia usiku ule kilikuwa kimelipiwa.
Akiwa amejilaza kitandani huku akipata wine, alifikiria jinsi atakavyompelekesha MJ ili apate kitu kingine cha thamani. Alijikuta akikaa muda mrefu bila MJ kutokea, kitu kilichomshtua sana. Alipopiga simu ya MJ haikuwa hewani aliendelea kumsubiri. Muda nao ulikatika alijikuta akikaa zaidi ya saa nne bila kuonekana.
Hasira zilimpanda kuamua kuondoka, wazo la kurudi nyumbani hakuliafiki aliamua kwenda kwa Shuku ili akamalize hasira zake. Kama kawaida alimkuta Shuku amejilaza kwake.
“Vipi mbona ghafla?” Shuku alishtuka kumuona Lily muda ule.
“Nimekukumbuka mpenzi wangu.” Lily alizunga
“Karibu.”
“Asante, Shuku nakupenda nimelala usingizi umekataa kabisa nikaona noje nilale na wewe mpenzi wangu.”
“Mmh! Haya.”
“Mbona unaguna mpenzi?”
“Nimefurahi kuona upendo umerudi.”
“Vipi shemu yupo?”
“Alikuwepo, ooh! Kweli ametoka si unamjua mtu wa totoz alikuwa na mtu wake kamsindikiza.”
“Ametoka saa ngapi?”
“Sasa hivi, nina imani hata dakika kumi hazijapita ungewahi ungemkuta.”
“Mmh!”
“Vipi mbona unaguna?”
“Ndugu yako ataukwaa anapenda sana wanawake.”
“Ndiyo hobi yake, unafikiri na mimi ningekuwa kama yeye ningeteseka hivi.”
“Jamani usiseme hivyo, mbona mi yamekwisha mpenzi wangu.”
“Mmh! Sawa, ila ikijichanganya nami naanza kazi ya kuoa usiku kuacha asubuhi.”
“Usifanye hivyo mpenzi wangu, Shuku nakupenda sana.”
“Haya mama karibu.”
Waliingia chumbani huku Lily akizidi kufura kwa hasira kutokana na kitendo cha MJ kumpaki hotelini kumbe ana wanawake wake. Moyoni aliapa kumshikisha adabu MJ kwa kitendo alichomtenda.
Alipokuwa akivua nguo ili aende bafuni simu yake iliita, alipoitazama alikuwa MJ aliikata huku ajifyonza. Kitendo kile kilimshtua Shuku na kuhoji.
“Vipi mbona hivyo?”
“Si huyu dada nimemwambia nimekuja kwako ananipigia.”
“Si umpokelee unajua amepiga kwa sababu gani?”
“Achana naye mi ndiye ninaye mjua ni msumbufu.”
“Mmh! Haya mi simo.”
Baada ya muda ujumbe uliingia aliufungua na kuusoma:
“Bebi upo wapi? Mi nimeishafika.”
Kauli ile ilimuudhi sana Lily na kuona kumbe alitangulizwa hotelini ili alishwe makombo. Kwa hasira aliizima simu kabisa na kuuapia moyo wake kesho kumfanyia vimbwanga ili ajue naye ana thamani mbele ya mwanaume yeyote.
Walikwenda bafuni kuoga na kurudi kitandani, moyoni Lily aliuapia moyo wake kumpa Shuku penzi zito litakalo mchanganya na kuiomba ndoa ili kuepukana na MJ aliyekuwa akimnyanyasa kimapenzi tofauti na Shuku. Walipofika kitandani baada ya maandalizi mchezo ulianza huku Lily akifungua kitabu cha dazeni burudani zenye utamu usoisha hamu kwa kujituma huku akilalamika muda wote kama anaonewa kitu kilichokuwa kigeni kwa Shuku na kumfanya apagawe zaidi.
“Shu..shu..ku.”
“Mmh!”
“Jamani niitikie basi mpenzi.”
“Bebi unanirusha stimu maana leo umekuja na machejo mapya yaani mimi mwenyewe hoi raha mwanzo mwisho.”
“Niitikie basi..Shu..shu..ku.”
“Mmh!”
“Jamani mbona hivyo hutaki kuitikia mpenzi wangu?” Lily alilalamika kwa sauti ya kumung’unya sukari guru.
“Bebi nikiitikia mtamu atadondoka.”
“Shuku muongo utamu upo juu au chini?”
“Kote kote mpenzi mdomoni kumezidi huwezi kuimba huku unatafuna karanga mpenzi.”
“Niitikie basi usikie nataka kukwambia nini?”
“Haya niite.”
“Shu..shu...aaah.. gari limenaelekea bondeni nidake mpenzi wangu naanguka peke yangu,” Lily alipiga kelele baada ya kwenda markiti bila kutalajia.
Shuku aliwacha atatalike kama kakalia msafara wa siafu, baada ya kutulia aliendelea na safari huku akipata muda wa kumuuliza Lily.
“Mpenzi.”
“Abee.”
“Vipi?”
“Safi.”
“Mbona uniiti tena?”
“Nani alikuwa akikuita?”
“Si wewe.”
“Mimi nimekuita?”
“Ndiyo”
“Muongo! Nimekuita ili iweje?”
“Mmh! Basi.”
Shuku aliendelea kupiga kasia kutoka maji mafupi kuyafuata maji marefu ambayo yalikifanya chombo kianze kuyumba kwa mawimbi kwa kwenda juu na kushuka chini.Kila safari iliyokuwa ikiendelea na ufundi wa Shuku kupiga kasia Lily alikuwa akizidi kukolea ghafla tui lilikolea nazi na kuanza kutatalika tena.
“Shu..shuku mpenzi wangu.”
“Mmh!”
”Shuku niitikie mpenzi wangu nikwambie kitu.”
“Niambie.”
“Nitakwambiaje bila kuitikia.”
“Niite basi.”
“Shuuuku.”
“Naam.”
“U.u.na..nipenda?”
“Ndiyo.”
“Muongo.”
“Kweli nakupenda Lily.”
“Mbona unioi?”
"Nitakuoa mpenzi wangu.”
“Lini?”
“Bebi unazimaliza raha zangu,”
“kwa vipi?”
“Stimu zinapanda unazitibua Lily.”
“Ni..ni..sa..sa..me..me..meeeee....li,lingine tena jamani Shuku yaani leo hata sijui mpenzi wangu.”
Lily alitetemeka kama mgonjwa mwenye degedege na kutulia akiwa amekwenda markiti kwa mara ya pili mfurulizo huku mwanaume kwake mambo baaado kabisa. Mpaka mwanaume anakanyaga yai la kuku na kulipasua mtoto wa kike shughuli ilimkuta na kujikuta akifunua mdomo bila kutoa maneno kama samaki anayekunywa maji.
Kwa vile wote walikuwa wamechoka walipitiwa na usingizi mpaka siku ya pili Lily aliporudi nyumbani kwao. Wakati anatoka alikutana na MJ akitoka chumbani kwake alimkata jicho kisha alibinua midomo na kufyonza kisha alielekea nje kitu kile kilimshtua Shuku na kujiuliza kuna kitu gani kati ya mpenzi wake na MJ.
Wazo lake la haraka lilikuwa labda MJ alimtongoza Lily na kumtolea nje lakini hakutaka mawazo yake kuyaelekeza huko moja kwa moja aliamua kulifuatilia kwa siri.
Walipofika nje waliagana na Lily kurudi nyumbani kwao, njia nzima Lily alijikuta akizidi kumchukia MJ na kuapa moyoni kumkomesha kwa vitendo alichomtendea cha kumwita na kumwacha hotelini kumbe alikuwa na mwanamke mwingine.
Alipofika nyumbani alioneka mtu aliyekosa furaha japo penzi la Shuku lilikuwa mwana ukome. Dada yake alikuwa wa kwanza kuigundua hali ile japokuwa alijitahidi kuificha.
“Vipi mdogo wangu kulikoni?”
“Kawaida tu dada.”
“Hapana haupo vizuri umetibuana tena na shemu nini?”
“Yaani bora tungetibuana kuliko anachoendelea kunifanyia.”
“Kipi tena?”
“Si cha kuita hotelini asitokee na kunifanya kama sina pa kulala.”
“Sasa kama alikuita hotelini asitokee kwa nini usirudi nyumbani kulala. Nawe unapenda mtu hatokei unalala mpaka muda huu.”
“Dada si yamejirudia yaleyale ya Shuku kuokoa jahazi, tena sasa hivi sijui Shuku anajua natembea na MJ yaani penzi analonipa toka nivunje ungo sijawahi kupewa leo nilichanganyikiwa. Yaani kama ndiyo nimo ndani ya ndoa lazima nidai taraka ili ikalifaidi.”
“Mmh! Usiniambie.”
“Dada Shuku anayajua mapenzi anajua apige wapi kumsambalatisha mwanamke.”
“Wacha weee!”
“Nilipanga kumpagawisha lakini nimepagawa mimi.”
ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA

KAMA ULIKOSA SEHEMU ZA NYUMA SOMAHAPA
SOMA SEHEU YA KWANZA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
SEHEMU YA 2: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html
SEHEMU YA 3:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-03.html
SEHEMU YA 4:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-04.html
SEHEMU YA 5==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-05.html
SEHEMU YA 6: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-06.html
SEHEMU YA 7==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-07.htm
SEHEMU YA 8==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-08.html
SEHEMU YA 9==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-09.html
SEHEMU YA 10 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-10.html
SEHEMU YA 11 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-11.html
SEHEMU YA 11 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-12.html

:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.

Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.
a kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.

No comments

Powered by Blogger.