TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 06
“Jamani mimi ni hadhi ya Shuku?” aliwauliza mashoga zake kwa sauti ya juu waliokuwa mbali kidogo na yeye.
“Ha! Ndicho alichokusimamishia?” waliuliza.
“Eti jamani mbona leo kajua kunitia nuksi, najiona kama nimekutana na paka mweusi.”
Yalikuwa maneno yaliyomdhalilisha Shuku na kujiona kama kajipaka kinyesi, Shuku akiwa ndani ya gari aliyawaza yale yaliyomfanya awaogope wanawake wazuri kama ukoma. Alijiuliza siku ile yule demu na shoga zake waliomtoa nishai wakimuona yupo vile watasemaje.
Alikwenda kupiga picha na kuzipeleka kwa mkuu wa usalama barabarani, kisha alirudi uswazi kwake kulipa kodi ya nyumba. Alipokaribia nyumba aliyokuwa akiishi alifungulia muziki kwa sauti ya juu na kuwafanya wote kuliangalia lile gari.
Alilifunua na kuwafanya wote waliokuwa wamekaa akiwemo Suzy kulishangaa lile gari lilionekana la ajabu mtaani,alilipaki pembeni ya nyumba anayoishi.
Alitulia kidogo kabla hajateremka kuwaacha watu washangae kwa muda kisha alilifunga na kutulia tena kabla ya kuteremka huku kila mmoja akimtumbulia macho. Suzy na kampani yake walijiuliza zungu la unga limetoka wapi. Baada ya kutembea kuelekea ndani wote walishtuka kumuona Shuku.
“Suzy yule si Shuku?”
“Hapana Shuku awe vile labda ndugu yake.”
“Hapana ni Shuku.”
“Makubwa mbona tutakoma, gari na pamba kali katoa wapi?”
“Najua?”
“Mmh! Inawezekana alinitongoza akijua mimi ni hadhi yake, maskini sikujua,” Suzy alijikuta akijilaumu kumkataa Shuku.
“Dharau zako shoga, lakini bado una nafasi, sasa zamu yako kujipendekeza kwake,” shoga yake alimshauri.
“Naona aibu.”
“Aibu ya nini wakati ni jambo la kawaida bila kuwa kauzu mjini hatukai.”
Wakati wakijadiliana na hali ya Shuku, ndani walimpokea kwa mshtuko.
“Jamani hodi,” Shuku aliingia kwa mama mwenye nyumba.
“Ha! Shuku?” alishtuka kumuona alivyolipuka.
“Ndiyo mimi mama.”
“Ha! Mwanangu siamini!”
“Amini mama ni mimi.”
“Karibu mwanangu.”
“Asante, sasa mama mi si mkaaji kile chumba alichohama mtu jana kina mtu?”
“Hakina baba.”
“Sasa mama, sasa hivi nitalipia miaka miwili na deni ulilokuwa ukinidai.”
“Hakuna tatizo baba, tena utakuwa amenisaidi maana hali ilikuwa tata.”
“Ila chumba changu kitakuwa na vitu vyangu nami nitakuja siku moja moja, lakini sasa hivi nina maisha mengine kabisa.”
“Jamani Shuku sasa hivi unaishi wapi?”
“Utajua muda si mrefu mama.”
Shuku alimuhesabia fedha ya miaka miwili na deni kisha alimpa elfu ishirini ya soda.
“Asante mwanangu, Mungu akuzidishie huku uliko.”
“Atuzidishie wote, ila baada ya muda nitakuja kubadili vitu vya ndani, na hii fedha atampa salmini amihamishie vitu vyangu.”
Shuku baada ya kulipia pango miaka miwili aliagana na mama mwenye nyumba na kuelekea kwenye gari lake. Wakati anatoka aliwakuta wale wanawake wakisumbiri kwa hamu wamuone kwa mara nyingine, Shuku aliyelipuka pamba za nguvu na kamba nzito shingoni, chini alikuwa na raba kali. Kwa jinsi alivyokuwa hakukuwa na mwanamke yeyote anayeweza kusimamishwa na Shuku akakataa.
Kabla ya kutoka nje alivaa miwani ili aweze kuwasanifu waliombele yake, alipofika mbele ya gari lake aliwatazama wale wasichana macho yalivyowatoka kama wameona meli barabarani, Shuku alichekea moyoni. Kabla ya kuondoka walitokea washkaji zake waliokuwa wakirudi toka kwenye mihangaiko, kwanza walimpita bila kumjua alipowaita ndipo waliposhtuka na kushangazwa na maajabu ya dunia.
“Shuku ni wewe?”
“Ni mimi ndugu zangu.”
“Mbona kama njozi ni asubuhi tulikuwa pamoja ajabu sasa hivi umekuwa kama mtu wa hadithini?”
“Ni historia ndefu ila tutazungumza wiki endi.”
“Sasa tuachie basi mshiko, yaani baada ya kuachana asubuhi siku ya leo imekuwa na gundu tupu.”
“Poa wangu,” Shuku aliingiza mkono mfukoni na kutoa fedha alizozihesabu kwa kuzionesha ili wale wasichana waone na kuhesabu elfu therasini na kumpa kila mmoja elfu kumi kisha aliwaaga rafiki zake.
“Sasa washikaji ngoja nirudi nikapumzike, nilikuja kulipia chumba changu pia nilipitia kwa mkuu wa trafiki kwa ajili ya leseni si mnajua sina gamba sitaki nikitembea na gari nipate usumbufu.”
“Mmh! Hatukuwezi, sasa ndo upo anga zipi?”
“Mtajua tu washikaji zangu nikija jumapili mtaelewa.”
Baada ya kusema vile aliingia kwenye gari, kabla ya kuondoka alilifunua gari na kuwafanya rafiki zake wapige kelele za mshangao.
“Wawooo, si mchezo mwana una kitu cha nguvu mwaka huu wanga lazima wazime zao.”
“Poa washkaji baadaye,” Shuku alisema huku akiwasha gari aondoke. Wakati Shuku akiagana na rafiki zake ili aondoke zake Suzy na shoga zake walikuwa kwenye kigagaziko kikubwa wafanye nini ili kumnasa Shuku.
“Sasa jamani nitafanyaje na Shuku ndio anaondoka?”
Suzy aliuliza baada ya kuchanganyikiwa hasa akikumbuka kuna siku alimtoa niashai mbele za watu na mashoga zake. Alijiulaumi bora angemkatalia kistaarabu kuliko alichomfanyia na siku ile aliamini kabisa hawezi kumsikiliza.
“Shoga jitoe akili muwahi kabla hajaondoka na kumwita mpenzi, Suzy unalipa hawezi kuchomoa.”
“Kweli eeh!”
“Muwahi kabla hajageuza gari.”
Suzy alitoka mbio kukimbilia gari la Shuku, alipolikaribia alimwita.
“Shuku.”
Shuku kabla ya kuitikia aligeuka kumtazama na kumuona ni Suzy alichekelea moyoni na kuona alichokitaka kimefanikiwa. Suzy alilisogelea gari huku akimwita kwa sauti.
“Shuku mpenzi.”
Shuku alisimamisha gari na kumsubiri anataka kumwambia nini.
“Shuku mpenzi mambo?”
“Poa, vipi unasemaje?”
“Jamani Shuku mpenzi maneno gani hayo, siku ile uliponitongoza nilijilaumu kwa maneno niliyokutolea, lakini lazima nikueleze ukweli. Shuku nimegundua wewe ni mwanaume mzuri.”
“Asante.”
“Kwa hiyo?”
“Mimi si taipu yako.”
“Jamani Shuku yale yalikuwa maneno tu, lakini ukweli kama ulivyosema ulikuwa na haki ya kuyasema yale.”
“Ni kweli, lakini mimi sasa hivi mademu wangu wa geti kali si ninyi kunguru wa Zanzibar hamfugiki mmezoea kula utumbo wa kuku nikikupeleka Masaki utachafua.”
“Ha! Shuku?”
Shuku hakujibu kitu alilifunga gari kwa juu na kuwa ndani kisha alimtimulia vumbi na kumwacha Suzy amesimama kama sanamu huku akiaibika mbele za watu na shoga zake kutokana na kuoneka matawi ya juu mwanaume yeyote apindui kwake. Ilikuwa aibu ya mwaka kwa Suzy kumtokea, alisimama kwa muda akiitumbulia macho gari mpaka lilipopotea. Kurudi miguu ilikuwa mizito, kwa aibu iliyomkuta alitamani ardhi ipasuke immeze lakini haikuwezekana. Shoga yake mmoja alimfuata na kumshika mkono na kumuondoa alipokuwa amesimama kama kagandishwa na gundi.
“Pole dada.”
“Mmh! Siamini yaani Shuku ndiyo kaniadhiri namna hii tutaona, nipo radhi hata kumroga hawezi kunidhalilisha kiasi hiki.”
“Achana naye si unajua tena maskini akipata matako hulia mbwata.”
“Yaani wee acha tu sijui aibu hii utafutika lini, hivi Mwaju mtaani watu watanitazamaje kwa kitendo cha Shuku?” Suzy alisema huku akitokwa na machozi ya uchungu.
“Lakini dada usisahau muosha huoshwa, kwa kweli hata mimi sikufurahi siku ile ulivyomdhalilisha Shuku.”
“Lakini kwa wakati ule ningemuweka wapi na hali yake ile hata angetupwa jalalani asingeliwa na paka?”
” ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA
KAMA ULIKOSA SEHEMU ZA NYUMA SOMAHAPA
SOMA SEHEU YA KWANZA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
SEHEU YA 2: >>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html
SEHEU YA 3: >>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-03.html
SEHEU YA 4: >>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-04.html
SEHEU YA 5:>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-05.html
: Utamu ndio kwanza unazidi kukolea. Bado sehemu kibao kuweza kuisha chombezo hili la aina yake . Kamwe usithubutu kusimuliwa hii simulizi ingia ujisomee mwenyewe hapa hapa uwanja wa simulizi pekee.
:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.
Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.
TUKUTANE HAPA SIKU YA KESHO

Post a Comment