CHOMBEZO: MPANGAJI SEHEMU 21
“Okey.Nitafanya hivyo”.Nilimjibu na kuingia ndani na kumwacha
yeye amesimama pale gizani.
Usiku huohuo nikiwa napanga nguo zangu ili kesho asubuhi na mapema niondoke,ndipo simu yangu ikaita.Nilipoangalia,alikuwa ni Gasper.
“Niambie Master P.Mtoto wa Vitoto”.Alianza Gasper kwa furaha.
“Dah! Huku mambo mwamala kaka”.Nilimjibu nikimaanisha mambo yameharibika.
Usiku huohuo nikiwa napanga nguo zangu ili kesho asubuhi na mapema niondoke,ndipo simu yangu ikaita.Nilipoangalia,alikuwa ni Gasper.
“Niambie Master P.Mtoto wa Vitoto”.Alianza Gasper kwa furaha.
“Dah! Huku mambo mwamala kaka”.Nilimjibu nikimaanisha mambo yameharibika.
“Kivipi kaka”.Naye aliniuliza.
Huku nikiwa naongea kwa sauti ya chini,nikamjibu.
“Eee bwana Shei ana mimba, kaka”
“Acha bwana,ya nani?”.Naye aliniuliza.
“Yangu kaka”.Nikamjibu.
“Hapo sasa kaka.Halafu nina taarifa mbaya zaidi kwako kuhusu kazi ya baba yake”.Naye akazidi kunipa mshawasha.
“Eheee,embu niambie”.
“Baba yake FBI”.Aliniambia.
“Una maana gani?”.Niliuliza.
“Baba ya Jasusi kaka.Jitu la CIA lile”.Alizidi kunipa hamasa Gasper ya kutaka kujua maana ya maneno yake.
FBI ni
shirika la kipelelezi la Marekani huku CIA ni shirika la Kijasusi la Marekani
pia.
Mashirika
haya yanafanya kazi aina moja lakini katika majukumu tofauti.Kazi zikiwashinda
FBI zinaenda kwa CIA,na kazi zikishindwa na CIA,zinapelekwa FBI.Sasa naambiwa
kuwa baba wa Shei ni Jasus sijui FBI,halafu nimempa mimba mtoto wake.
“Bado
sijakuelewa Gasper.FBI si huko Marekani kaka?”.Bado nilitaka kupata ufafanuzi
halisi wa maneno yale.
“Kazi ya FBI
si waijua?Au CIA si wajua kazi zao hawa?”.Aliniuliza Gasper.
“Ndio
kaka.Hao ni wapelelezi”.Nikamjibu huku nikiwa na bonge la mtetemo.
“Basi na
huyo dingi ni mpelelezi.Yupo usalama wa taifa huyo mzee wa hapa Tanzania.Hapo
kanisani ni kujivalisha ngozi ya kondoo tu! Ili tusishtukie ishu.Ila ukweli
dingi ni FBI”.Aliongea Gasper na nilijihisi mkojo kutoka baada ya kujua baba wa
Sheila yupo usalama wa taifa.
“Kaka…..Kaka……Kaka
mbona kimya?”.Sauti ya Gasper ilisikika lakini nilishindwa kuipa jibu na
niliamua kukata simu tu!.
Baada ya
kuikata ,nikaanza kupanga nguo zangu haraka haraka na kuweka vyeti na vitu
vyangu muhimu mahala pake. Kisha nikakaa kitandani na kuvuta pumzi ndefu huku
nikiomba kesho ifike haraka niondoke bila familia ile kuniona.
Baada ya
mawazo na kusali sana,sala ambazo sijui zilikuwa zinaenda kwa nani,lakini
nilikuwa naomba hadi mizimu ya mabibi inisaidie.Nilipitiwa na usingizi mzito
ambao mwisho wake ulikuwa ni kesho yake saa kumi na moja asubuhi.
Ni kaka
ndiye aliyekuja kuniamsha na kunitaka nijiandae haraka kwani gari linaondoka
saa kumi na mbili,saa moja kuanzia pale nilipoamka.
Nilinyanyuka
na kwenda bafuni ambapo sikutumia muda mwingi sana.Na hadi dakika kumi na tano
zinaisha tayari nilikuwa mezani napata kifungua kinywa kwa mwendo wa haraka.
Baadae
nilisikia kaka akigonga mlango wa baba mwenye nyumba. Dakika kama moja,tayari
mlango ule ulifunguliwa na mzee yule alikuwa uso kwa uso na kaka.
Baada ya
salamu,niliitwa na mimi ili niage kabla sijaondoka.
Mwili
ulikuwa tayari ushaanza kulowa kwa jasho licha ya baridi kali iliyokuwa inapiga
asubuhi ile.Macho ya mzee yule yalivyokuwa yananiangalia,waweza sema huyu mzee
anataka kukurukia ili akutafune mzima mzima. Nilikuwa nimekaa kwenye kochi moja
kumwelekea yeye,hivyo uso wake niliuona moja kwa moja.
“Kwa hiyo
kijana unaondoka?”.Aliniuliza swali hilo mzee yule baada ya kuniona nimekaa
sawia kwenye kochi mojawapo la mle
ndani.
“Ndiyo
mzee,nadhani MUNGU akipenda tutaonana”.Nilimjibu kiuhakika huku nikiwaza
itakuwaje kama tayari kishajua kuwa mimi ndiye mtuhumiwa anayenitafuta kwa muda
sasa.
“Okey.Basi
vizuri.Nashukuru sana kwa yote tangu
ulipokuja hapa.Na kama una cha kuongezea,huu ndio muda wake.Usiogope”.Mzee
aliniambia maneno ambayo yalinifanya nikae njia panda nikijiuliza yana maana
gani?.Ina maana mzee anajua ila anategea mimi nimwambie kuwa nimempa bend
Shei?Au anataka kunitega ili nijitaje kuwa nimempa kitu mwanae.
Maswali hayo
nilijiuliza haraka sana kichwani mwangu,na jibu nililolipata ni kwamba huyu
mzee ananitega tu! Ili nijitaje.Sasa kaumia,sijitaji wala nini.
“Hapana
mzee,sina chochote zaidi ya kukuomba uniagie kwa wengine”.Nilimwambia hivyo na
kumfanya atabasamu kwa tabasamu la upande mmoja.Kisha akafungua kinywa chake.
“Mimi siwezi
kukuagia bwana.Ngoja niwaite uagane nao”.Alisema mzee yule na kutaka kuwaita
wanawe ili waniage.Lakini kwa kuwa kaka alikuwepo na anaenda na
muda,alisimamisha zoezi hilo na kumwambia mzee yule kuwa tunachelewa.
“Okey.Kama mnawahi,sawa.Ila ningependa huyu
awaage hawa watoto”.Mzee yule bado alikuwa anasisitiza ombi lake.Lakini hadi
muda ule tunaongea,tayari zilibaki dakika ishirini za mimi kuripoti kituoni kwa
ajili ya kurudi zangu Morogoro.
Hatimaye
nikabeba mizigo yangu kwa ajili ya kwenda kituo kikubwa cha mabasi pale
Arusha.Kaka akiwa kwenye usukani na asiye na wasiwasi juu yangu,alikuwa
anacheka sana jinsi mzee yule alivyokuwa anang’ang’ania niwaage watoto wake.
“Tuambiane
dogo.Ndiyo baba mkwe nini?Maaana alivyokung’ang’ania,dah!Kama ruba vile”.Kaka
alikuwa anaongea huku akifuta machozi kwa sababu ya kucheka.
Mimi
nilikuwa na mashaka sana,na hata cheko yangu niliyoitoa ilikuwa na woga mwingi
ndani yake.
“Hamna.Si
wajua hawa wazee walivyowaswahili”.Nilimjibu kaka ila moyoni nilitamani sana
nimwambie nini kinachoendelea.Sema sasa nilihisi ataniona wa ajabu na
atakasirika sana kwa kitendo nilichokifanya kwa Sheila.Mtoto ambaye Mzee Donyo
alimuona kama mkombozi wa familia ile hapo baadaye kwani dada mtu,tayari
alishakubuhu kwa wanaume.
“Dogo sema
bwana.Sisi ni kaka zako”.Kaka alizidi kunisisitiza lakini kwa utani mwingi hadi
nikaona ni bora nifunguke tu!.Liwalo na liwe.
“Bro,pale
bwana kuna matatizo makubwa tu!Ndo maana unaona mzee kanikazia niwaage wale
watoto”.Nilianza hivyo kumwambia kaka huku bado macho yake yakiwa barabarani
kuelekea kituo cha mabasi.
“Matatizo
gani dogo tena”.Kaka aliniuliza.
“Ni
Sheila”.Nikamjibu kifupi tu!.
“Sheila
kafanyaje sasa,mbona hauwi spesific?”
“Sheila ana
mimba yangu bro”.Nikamjibu na kugeukia dirishani ili nisione sura yake
itakavyobadilika.
Kinyume na
mategemeo,alionekana hata hajashtuka na zaidi alicheka sana.
“Nilijua
tu!Utakuwa wewe.Ila nikawa nakusubiri nione na mimi kama utanificha,ha ha ha
haaa.Dogo una kazi sana”.Alicheka kaka na kuniambia maneno hayo ambayo kwangu
yalizaa mawazo mengine.
“Sasa na
kazi gani Bro?”.Ilibidi nimuulize.
“Wewe
unadhani unaweza kula vya watu na kuondoka mjini hivi hivi?”.Kaka aliniambia
kwa mafumbo.
“Sijakuelewa
kaka una maana gani”.
“Ukiondoka
hapa Arusha bila tatizo,kweli mizimu yako itakuwa mikali sana.Niamini
nachokwambia”.Kaka alinijibu na kuzidi kusababisha mimi tumbo la kinyesi
kunibana hasa nikifikiria kazi ya mzee yule.
Nilipumua
pumzi ndefu na kukaa kimya kwa mawazo ambayo sidhani kama alikuwepo wa
kuyawazua muda ule.
“Tatizo lako
wewe dogo hujali kitu hata kidogo.Hukuona shida kuwachanganya wale mabinti wote
na mbaya zaidi kwako dhana ikawa shida kuitumia kwa huyu mtoto tegemezi wa Mzee
Donyo.Sasa mimi sitaingilia masuala yenu,na ni bora palepale ungejitaja tu ili
yaishe”.Kaka alizidi kunipa mawazo na kunifanya sasa kile kinyesi kugonga hodi
kwenye boxer langu.
“Halafu wewe
isitoshe ni mjinga sana tena sana.Mimi pale naheshimiana sana na yule mzee,ila
kwa kuwa kwako ujana na maji ya moto,basi ukaamua kuwamwagia wengine.Sasa
uaminifu kati ya mimi na mzee yule,hamna tena.Unadhani mimi kwa sasa nitahamia
wapi?
Sijapanga
kabisa kuhama muda huu.Embu fikiria dogo,kwa nini umenifanyia hivyo?”.Kaka sasa
alibadilika na kuonesha wazi kuwa naye kachukia sana kitendo changu.Hakuishia
hapo,akaendelea.
“Nyumba
yangu ukaifanya nyumba ya ngono.Kitoto kidogo,miaka kumi na
tisa.Kisheila,kinaingia ndani na kufanya unyambilisi na wewe.Eti mnajidai
mmeoana wenyewe.Sasa kazi ni kwako.Mimi siingilii nakwambia”.Hadi kaka
anamaliza kuongea hayo,mimi nilishalowa jasho kama nimtoka mazoezini.
“Na
ninavyomjua mzee yule.Nadhani ukitoka hapo utakuwa umejifunza na umebadilika”.Kaka
aliniambia hayo wakati gari linaingia pale kituoni.
Baada ya
kuhakikisha nimepanda kwenye gari la wasafiri wa kwenda Morogoro,aliniaaga na
kuniambia nisali sana.
***********
Baada ya
dakika tano,gari lile lilianza kupiga honi likiashiria kuwa muda wake wa
kuondoka umewadia.Mimi nilifumba macho na kumshukuru MUNGU kwani safari ilikuwa
imeshaanza.
Tukatoka
getini,na kuingia kwenye barabara tayari kwa safari ya kwenda Morogoro.
Amani
ikanitawala kiasi chake baada kuona saa zima tunasafiri bila misukosuko.Usingizi
ukanipitia kamanda na kuona kuwa tayari nimemaliza kazi.
************
Nilikuja
kushtuka ghafla baada ya gari kupiga breki kali zilizofanya hata watu wengine
mle kwenye basi kupiga kelele za hofu na hamaniko.
“Huyu dereva
mshenzi nini.Anataka atuue wengine hapa?”.Aliongea mama mmoja mwenye mimba
baada ya breki ile.
Chombezo linazidikunoga hakikisha haikupiti hata siku moja.
:: Endelea ku LIKE PAGE YETU na ku COMMENT chombezo hili kali na lakusisimua.
:: Kwa wale watakaokuwa waki SHARE 100 wa kwanza nitawapa kipaumbele kwa kuwa TAG chombezo hili kila litakapokuwa likitoka litakuwa katika wall yao
MPANGAJI sehemu ya 21 itaendelea tena kesho HAPA.
Post a Comment