AZIZA WA FACEBOOK SEHEMU YA 06
Kwa sababu
aliniambia kwamba angekuja mpaka kwa Tandale Kwa Mtogole wala sikuwa na
wasiwasi, nilichokifanya ni kuelekea katika sehemu ya Mafyoso Camp ambapo
vijana wengi tulikuwa tukitumia kukaa na kutulia. Siku hiyo, mawazo yangu yote
yalikuwa juu ya msichana Aziza ambaye alitarajiwa kufika muda si mrefu,
sikutaka kumwambia mtu, nilichotaka kukifanya nilitaka kiwe sapraizi kwa kila
mtu mahali pale. Ilipofika saa tisa na robo alasili, simu yangu ikaanza kuita,
nikaipokea na kisha kuipeleka sikioni.
AZIZA:
Nimekwishafika hapa kwa Mtogole.
MIMI: Ok!
Unaiona hiyo njia ya vumbi kushoto kwako?
AZIZA:
Nimetokea huku Kijitonyama Sayansi.
MIMI:
Haina noma. Vuka barabara ya lami na kisha ingia katika barabara ya vumbi,
nyoosha, hapo mbele njia imegawanyika, panda na hiyo ya kushoto moja kwa moja
utanikuta mtu mzima nimejaa tele na wanangu.
AZIZA: Ok!
Nakuja.
Mapigo ya
moyo yakaanza kudunda, kila nilipokuwa nikimfikiria Aziza nilikuwa nakosa amani.
Nilikuwa nikijiangalia, japokuwa nilipendeza sana kama siku za sikukuu lakini
kwa macho yangu nilijiona bado kabisa. Kwangu, Aziza akaonekana kuwa kama
malkia fulani ambaye alikuwa akisubiriwa kwa mbwembwe zote kwangu. Macho yangu
hayakutulia, yalikuwa yakiangalia ile barabara ya vumbi ambayo ilionganisha
mpaka kwa Mtogole.
Baada ya
muda, kwa mbaliiiii niliweza kuliona gari moja dogo, Verrosa nyeusi, bila shaka
lilikuwa gari la Aziza ambalo alikuwa akilitumia. Ebwana sikufichi rafiki
yangu, nilipigwa na butwaa, nikakosa kujiamini. Sikutaka kuwaambia washikaji
juu ya Aziza kwa sababu unaweza kuwatambia halafu mwisho wa siku msichana
mwenyewe akaonekana kuwa si mzuri, mtu mzima ukaona noma.
Gari lile
likaendelea kuja, lilipofika karibu na pale tulipokaa, nikasimama na kisha
kulisimamisha kwa kupunga mkono. Kwanza washikaji wakaonekana kunishangaa,
hawakuwa wakifahamu kitu chochote kile kilichokuwa kikiendelea mahali hapo.
Nilibaki nikiwa nimesimama nje ya mlango hasa baada ya Aziza kusimamisha gari,
sikuweza kumuona kwa sababu vioo vilikuwa tinted. Aliposhusha kioo...MUNGU
WANGU!
Ngoja nikwambie
kitu rafiki yangu. Kati ya majini wote wanaojigeuza kuwa warembo na kuua
wanaume nyakati za usiku umewahi kuwaona? Kabla sijaendelea, ngoja nikwambie
kitu fulani. Mimi kama mimi nilikwishawahi kukutana na msichana ambaye alikuwa
jini nyakati za usiku, tena nakumbuka ilikuwa mkoani Kilimanjaro katika kipindi
ambacho kulikuwa na tetesi nyingi kuhusiana na majini ambao walikuwa wakiua
watu nyakati za usiku, bila shaka ilikuwa 2006 au 2007.
Usijiulize
nilijuaje kwamba huyo mwanamke alikuwa jini. Nilikutana nae usiku katika
kipindi ambacho nilikuwa nikielekea Majengo katika kipindi cha likizo,
nakumbuka ilikuwa saa mbili usiku, tulifunga shule na kuja Dar es Salaam
niliona ningetumia gharama kubwa.
Nilikutana
na huyo msichana, asikwambie mtu, alikuwa mrembo mkali sana, ukali wa msichana
yule jini sikuwahi kuuona kwa msichana yeyote yule toka nizaliwe, hata mrembo
wangu alikuwa haingii ndani.
Nilipopishana
nae, alikuwa akinukia manukato mazuri sana, nywele zake zilikuwa ndefu,
nilitamani kumsalimia, ila nilikuwa dogo, nadhani kama ningekuwa mkubwa, siku
hiyo na mimi lazima ningeuliwa tu...yaani ni LAZIMA. Unamwacha vipi msichana
mrembo unayepishana nae? Ukimwangalia, mwarabu si mwarabu, mzungu si mzungu na
mtu mweusi si mtu mweusi. Nilipopishana nae, nilipiga kama hatua tano,
nilipogeuka nyuma ili niangalie umbo lake la nyuma, kajazia vipi, sikumuona,
kilichofuata...ni kutoka nduki tu huku nikipiga kelele.
Nilipokuwa
nikiwangalia Aziza katika kipindi hicho nilikuwa nikimfikiria yule mwanamke
jini wa kule Kilimanjaro. Aziza, aisee Aziza....Mhh! Nadhani Eduado alikuwa
mchoyo, hakutoa sifa ambazo alistahili kuwa nazo Aziza, Aziza alikuwa msichana
mzuri sana, msichana ambaye....dah! Sijui nizungumze vipi.
Hahaha!
Kwanza kwa washikaji. Walipoona kwamba nimelisimamisha gari lile, wakataka
kuangalia ndani kujua kuna nani, nilikuwa nimewapa mgongo, mlango
ulipofunguliwa, Aziza akatoka nje...aiseeee. Si kwa watoto, watu wazima, mababu,
wala warembo wengine, wote wakabaki wakimshangaa Aziza, alikuwa mkali mpaka mtu
mzima nikawa najipa mapungufu.
Ukiachana
na zile sifa za uchoyo ambazo alikuwa amezitoa Eduado juu ya Aziza, acha
nikwambie jinsi alivyo, umtengeneze Aziza wako kichwani mwako na uone ni jinsi
gani alikuwa mrembo.
Kwanza Aziza
alikuwa Mpemba, kwa hapo sitaki nizungumze sana kwa kuwa wote mnaamini kwamba
wapemba wamebarikiwa kwa urembo, mtoto alionekana kuwa baba yake alikuwa
mwarabu, tena wa Dubai, mama yake alikuwa Mlangi, vuta picha mtu mzima. Mtoto
alikuwa na nywele nyingi sana, hapo ndipo nilipogundua mapungufu ya sifa za
Eduado. Mtoto hakuwa na nywele zilizoishia kwenye mabega, mtoto minywele
ilikuwa hiyooo mpaka mgongoni huku zikiwa zinang’aa sana. Uso wake ulikuwa
mwembamba ambao ulikuwa ukizungukwa na tabasamu pana ambalo lilikuwa
likiyafanya meno yake meupeeee kuonekana. Ukiachana na hayo, huyu mtoto alikuwa
na kidoti aisee, tena kile kidoto kilichokuwa karibu na pua, kilimfanya
kupendeza sana.
Ukiachana na
uso wake uliomfanya kuonekana kama malaika, umbo lake lilikuwa zuri sana. Huwa
wapemba ni kama waarabu au wachina, hawana makalio hayoooo tofauti na wanawake
wetu weusi, yeye alikuwa mwembamba wa wastani, kifua chake kilikuwa kimesimama.
Kwa sababu alikuwa amevaa sketi fupi kiasi, miguu yake haikuwa miguu ya bia,
ilikuwa miguu ya wastani kidogo. Kila nilipokuwa nikimwangalia, mtoto hakuwa na
kovu lolote lile, yaani alionekana kama katengenezwa kupitia Adobe Photoshop na
kisha kuja kwangu.
AZIZA: Wao
Ibraaaaaa.
Aliniambia kwa furaha na kisha kunikumbatia.
Watu wote ambao walikuwa wakimwangalia Aziza wakaanza kutushangaa, Aziza
alionekana kama mzungu, nilionekana kuokota embe katika mti wa mlimao au
kujenga nyumba kubwa angani. Aziza alikuwa akinukia vizuri sana, harufu ya
manukato yake ikanifanya nifall inlove zaidi na zaidi. Nilitamani kumbeba juu
juu. Warembo wa pale mtaani ambao walikuwa wakiniringia sanaaaaaa, katika
kipindi hiki walionekana kushikwa na wivu huku mioyo yao ikiukubali uzuri wa
Aziza.
MIMI:
Mzima wewe cheupe?
AZIZA:
Mimi mzima.
MIMI:
kweli nilipatia, sikutoka nje hata mara moja.
AZIZA:
Ulipatia nini?
MIMI:
Wanawake mnaoweka picha za midoli na maua huwa mnakuwa wakali sana.
AZIZA:
Kwani mimi mzuri?
MIMI:
Nilikuwa najiuliza kwamba hivi umezaliwa hapa duniani au umeshushwa kutoka
hukooooo.
AZIZA:
Hahaha! Acha hizo Ibra.
MIMI: Mtoto
unaonekana kuwa mrembo sana, mtoto una mvuto wa ajabu, mtoto unaonekana zaidi
ya malkia Cleopatra aiseee...dah! Ulivyonikazia kuwa na mimi sawasawa tu manake
ungenisababishia kifo.
AZIZA:
Kivipi?
MIMI: Mmh!
Hapa kifo nje nje aiseee. Tena bora ulivyokuwa na gari manake ungekuwa
unatembea kwa miguu, utawafanya hata wale wanaokwenda msikitini kuswali
wakatishe safari zao, utawafanya mpaka wale wanaokwenda kanisani kusali
wakatishe safari zao kwa muda wakuangalie wewe. Kama vitabu vya dini
vinavyosema kwamba ukimwangalia mwanamke na kumtani utakuwa umeshazini nae,
haki ya Mungu nina uhakika wewe umeshazini na watu wengi maishani mwako.
Umeshazini na mimi, umezini na wale marafiki zangu, umezini na wale mababu
waliokaa pale chini wakicheza bao, mbaya zaidi, umezini mpaka na wasichana
wenzako....hahahaha! Wamekusaga.
AZIZA:
Yaani yote hiyo kwa sababu wamenitamani?
MIMI:
Ndio. Hebu jiangalie, hivi unaweza kujilinganisha na nani? Hata Beyonce
haingiii, labda Alicia Keys ndiye anaweza kuifikia nusu yako.
AZIZA: Hahaha!
Ibra una maneno matamu. Hebu nisubiri kidogo niende hapo dukani.
AZIZA:
Unakwenda kununua nini? Hakuna pizza wala baga hapa Tandale.
AZIZA:
Hahaha! Hebu acha utani.
Huyu
Aziza. Aisee bora alivyoweka picha ya mdoli katika akaunti yake ya facebook
manake kama angeweka picha yake basi ingekuwa balaa. Mwendo wake ulikuwa ni wa
mapozi kupita kawaida, alionekana kutembea kwa tahadhali ardhini.
Nilichokifanya nikayapeleka macho yangu kwa washikaji waliokuwa pale kijiweni,
nilijua tu kwamba walikuwa na dukuduku mioyoni mwao.
JAFARI:
Kaka heshima. Kaka heshima yako...kuanzia leo...hauna mpinzani hapa mtaani aiseeee...duh!
MIMI:
Hahaha! Mtoto umemuonaje.
JAFARI:
Kwanza huyu mtoto umemtoa wapi?
MIMI:
Facebook.
JAFARI:
Duh! Kaka naomba na mimi uniunganishe manake dah!
MIMI: Kaka
mambo hayapo rahisi kama unavyofikiri. Mpaka nimempata huyu mtoto, nimepitia
kwenye mabonde, mito majabari mpaka wewe kumuona hapa. Usifikiri ukijiunga leo
kesho unampata, unaweza ukawa babu hujaambulia chochote.
ALLY: Kwani
huyu ni wa facebook?
MIMI: Yeah!
Tena yupo mpaka Twitter...yupo kotekote.
HUSSENI:
Ila huyu mrembo sio mgeni machoni mwangu, nadhani nilishawahi kumuona sehemu.
MIMI: Acha
uongo. Wapi?
ALLY:
Daah! Nshajichanganya. Kumbe kichwani mwangu ilikuwa inakuja picha ya Kajool,
yule mrembo muigizaji wa Kihindi.
MIMI:
Hahaha!
JAFARI:
Ila Ibra. Daah! Unapokuwa na mtoto kama huyu, hivi kweli unaweza kutembea nje
ya ndoa?
MIMI:
Kaka, sisi wanaume hatufai, hata upewe mrembo mzuri kama malaika, kesho unalala
na rafiki yake...hahaha!
AZIZA: Ibra.
MIMI:
Niambie (Huku nikimfuata)
AZIZA:
Tuondoke.
MIMI: Bila
ya kukanyaga nyumbani? Hebu acha zako, twende home.
AZIZA: Ibra...nataka
tuwahi nyumbani.
MIMI: Hata
kama. Twende mara moja tu.
Lengo
kubwa la kumtaka Aziza twende nyumbani lilikuwa moja tu, kutaka kuwaonyeshea
wale wasichana ambao walikuwa wakileta mapozi kwamba huyu msichana alikuja kwa
ajili yangu kwani kama nisingefanya hivyo, wangejua kwamba alikuwa mpita njia
ambaye alikuwa amesimama kutaka kuulizia kitu fulani. Kwa sababu alikuwa amelipaki
gari pembeni, nikawaambia washikaji waliangalie na mimi kuanza kuondoka na
Aziza kwenda nyumbani.
Watu
walikuwa wakinitolea macho, wengine walikuwa wakiniangalia kisiri na kunipigia
saluti. Aziza alionekana kukimbiza kupita kawaida, urembo wake ulikuwa ni
mkubwa kiasi ambacho hakukuwa na mtu aliyefikiria kama ningeweza kuja na
msichana mzuri kiasi kile.
AZIZA: Mazingira
ya huku nimeyapenda.
MIMI:
Umeyapendea nini?
AZIZA:
Yametulia sana. Halafu kumechangamka.
MIMI:
Hahaha! Nyie si mmezoea mazingira ya kwenu yapo kimya utafikiri jangwani.
AZIZA:
Yeah! Unajua kule sijui kupo vipi, huwa kunaboa kweli.
Katika
kipindi chote ambacho tulikuwa tukiongea huku tukielekea nyumbani, kichwa
changu kilikuwa kikimfikiria baba. Nilijua kabisa kwamba katika kipindi hicho
alikuwa nyumbani, kichwa changu kilikuwa kikifikiria uongo ambao nilitakiwa
kumpa, uongo ambao ungeendana na ukweli. Nilipofikiria kwa kipindi fulani,
nikapata jibu, nikapata kile nilichotakiwa kumwambia baba.
Kweli
tukafika home, majirani wote wakawa wananiangalia kwa macho ya kunishangaa,
Aziza, kwao alionekana kuwa tofauti sana, uzuri ambao alikuwa nao ulionekana
kuwa wa kipekee sana. Nikaufungua mlango, tulipoingia ndani tu, kizaazaa, baba
alikuwa kwenye kochi akiangalia televisheni.
Nikamkaribisha
Aziza, akamsalimia baba na kutulia kochini. Nikamwangalia baba huku lengo langu
likiwa ni kutaka kumsoma, hiyo ndio ilikuwa tabia ya nyumbani, muda mwingi watu
huwa tunasomana kabla ya kuongea kitu chochote kile. Baba akaonekana kufahamu
nilichokuwa nikikifikiria. Akaniwahi.
BABA:
Unaonekana unataka kuniambia jambo, halafu hilo jambo la uongo, hebu niambie
sasa nikusikilize.
MIMI:
Hahaha! Tatizo mzee Akilimia una presha sana. Wewe subiri kwanza, mbona unakuwa
na wasiwasi?
BABA: Huo
mtazamo wako unaoutumia kunitazama. Ok! Karibu mgeni. Sijui unatumia kinywaji
gani?
AZIZA:
Hapana. Nimeshiba.
BABA:
Kwani ukinywa kinywaji chochote utavimbiwa?
AZIZ:
Hapana. Nimekwishakunywa.
BABA: Ibra,
ni kweli anayoyasema?
MIMI:
Hapana. Hapo kakupiga fix.
AZIZA:
Hahaha!
BABA: Jisikie
huru. Uletewe kinywaji gani?
AZIZA: Maji
tu yanatosha.
MIMI: Ok!
Ila kuna maji ya chumvi...utakunywa?
AZIZA:
Mmmh! Maji ya chumvi?
MIMI: Sasa
unashangaa nini? Au haujui kama Dar es Salaam kuna bahari ya Indi?
AZIZA:
Niletee hata hayo nitakunywa tu.
ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA
KAMA UJALIKE PAGE YETU YA FACEBOOK, TUNAOMBA ULIKE KUPITIA HAPA CHINI ====>www.facebook.com/2jiachie
Post a Comment