ad

ad

Chadema chamtaka Waziri Membe asiwaingilie wasimamizi wa uchaguzi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, hana mamlaka ya kuwatisha wasimamizi wa uchaguzi na kumtaka awaache wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria na kanuni.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Naibu katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika, alisema kuwa serikali haitakiwi kuwatisha wasimamizi wa uchaguzi kwa kuwa ni wajibu wao kufanya kazi yao bila vitisho.
 
Alisema Membe alichokifanya ni matumizi mabaya ya nafasi ya uwaziri katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi .
Membe kama kada wa CCM ana haki ya kufanya mkutano wa hadhara ama kufanya mkutano na kueleza kuwa CCM itashinda huku moyoni akijua itashindwa kwa kishindo hilo ana haki lakini matumizi mabaya ya nafasi ya uwaziri katika kipindi cha uchaguzi kuwaita waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa na kuwatisha,
 
Alisema kama Membe hakuwa na nia mbaya katika mkutano huo  angejiweka mbali na uchaguzi ama kumuachia katibu wake azungumze. Hata hivyo, alisema sasa hivi mawaziri na Rais Jakaya Kikwete wanapiga kampeni za mgombea urais Dk. John Magufuli kwa kutumia kofia ya urais kujaribu kupiga bao la mkono kudhibiti mafuriko ya mabadiliko.
CHANZO: NIPASHE
Powered by Blogger.