Baracka De Prince ajitenga na Masogange
Boniphace Ngumije
Msanii
wa muziki, Baracka Endrew ‘Baracka De Prince’ amefunguka kuwa kufuatia
skendo iliyokuwa inamkabili ya kutoka kimahaba na Video Queen maarufu
Afrika, Agness Gerald ‘Masogange’ ameamua kujiweka naye kando mdogomdogo
ili kuepusha maneno kutoka kwa wambeya.
Akichonga na Ijumaa
juzikati, Baracka alisema anajua watu wanahisi ‘anabanjuka’ na ‘mtoto’
huyo kutokana na ukaribu wao hivyo ameona ni vyema afanye liwezekanalo
ili kuondoa mawazo hayo kwa watu.
“Kiukweli
yule wala siyo demu wangu na kwa kuwa huwa sipendi manenomaneno
yasiyokuwa na ukweli, nimeamua kupunguza ukaribu na Masogange na hata
picha zake nyingi Instargram nimefuta na yeye nilimwambia afanye hivyo
akakubali,” alisema Baracka.

Post a Comment