BARCELONA YAONYESHA JEURI YA FEDHA, YAWEKA PAUNI MIL 72 MEZANI KUMNYAKUA SUAREZ ...SANCHEZ AITAKA ARSENAL
LIVERPOOL na Barcelona zinatarajiwa kuingia kwenye maongezi mazito baada ya miamba hiyo ya Hispania kuweka mezani ofa ya pauni milioni 72 ili kupata saini ya mshambuliaji Luis Suarez (pichani juu).
Alex Sanchez
Dau hilo ni pungufu kidogo kwa pesa inayohitajiwa na Liverpool (pauni milioni 80), lakini ni wazi kuwa safari ya Suarez mwenye umri wa miaka 27 kwenda Barcelona imekaa pazuri.
Mwanzoni Barcelona ilitaka kumtumia mchezaji wake Alex Sanchez kama sehemu ya mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez lakini winga huyo wa Chile alikataa mpango huku akiwa na utashi wa kwenda Arsenal.
Habari za uhakika zikasema Sanchez mwenye thamani ya pauni milioni 30, alikuwa hakubaliani hata kidogo na mpango huo.
Hiyo inamaanisha kuwa njia pekee iliyobakia kwa Barcelona kumpata Suarez ni kutoka pesa kamili.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekuwa akiweka wazi utashi wake wa kumsaini Sanchez mwenye umri wa miaka 25 ili kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo ushambuliaji.
Watu wa karibu na Sanchez wanadai nyota huyo angependa kuishi London, jambo linaloiacha Arsenal kwenye nafasi nzuri ya kumnasa.
Via Saluti 5.com


Post a Comment