Inakuwaje mrembo mambo safi ampende kijana hohehahe?soma hapa.
Mpenzi msomaji wangu, mapenzi ni kitu cha ajabu sana, uajabu wake uko
katika mazingira tofauti lakini hili ninalotaka kulieleza leo ni pale
mtu anapotokea kumzimikia mtu fulani ambaye katika mazingira ya kawaida
watu wasingetarajia iwe hivyo.
Nasema haya nikimaanisha kwamba, katika hali ya kawaida tulitarajia binti kutoka katika familia bora, mwenye mvuto wa kimapenzi kutokuwa tayari kuwa na uhusiano na mwanaume anayetokea kwenye familia masikini asiye na mbele wala nyuma.
Lakini kinyume chake tunashuhudia mabinti warembo ambao mambo yao yako safi wakitokea kuwazimikia wanaume ambao ni masikini wanaopoteza siku zima wakipiga stori kijiweni na ukiwauliza watakuambia mioyo yao ndiyo imetokea kuwapenda na hawako tayari kuwakosa.
Miongoni mwa wasichana hao wapo ambao familia zao hufikia hatua ya kuingilia kati na kueleza kuwa, hawako tayari kuona binti yao akiwa katika uhusiano wa kimapenzi au kuolewa na mtu ambaye ni fukara, lakini kuonesha mapenzi yalivyo ya ajabu, msichana anaweza kukataa na kueleza kuwa, endapo atalazimishwa kuachana na mwanaume aliyempenda kutoka moyoni mwake, bora asiendelee kuishi!
Achilia mbali hilo, wapo wanaume ‘mahandsome’, wenye uwezo kifedha ambao katika mazingira ya kawaida tulitarajia kuwaona wakiwa na wapenzi wakali lakini ashakum si matusi, unakuta kijana huyo yuko na jimama au binti ambaye hana shepu, hana sura yaani yupo yupo tu lakini mwanaume anakuambia kwake ndiyo kafika, hasikii la kuambiwa. Jamani hayo ndiyo mapenzi! Mapenzi hayana macho, ukishapenda umependa bila kujali huyo uliyempenda yukoje.
Ndio maana katika mazingira hayo unakuta baadhi ya watu wakiwasema wenzao kutokana na sampuli ya wapenzi walionao. Utawasikia wakisema maneno kama vile, “Huyo nanii naye, mwanaume gani sasa yule aliyenaye? Utadhani kalazimishwa kupenda! yaani na uzuri wake wote kaamua kuolewa naye?” Wapo wanaosema maneno hayo huko mtaani.
Wengine hawaishii kuwateta tu wenzao bali hudiriki hata kuwaambia laivu kwamba, wapenzi walionao hawaendani nao. Jamani hivi hamjui kwamba kibaya kwako kizuri kwa mwenzako? Tambua kwamba, unayemuona si mzuri kwako wapo wanaomfukuzia lakini hawampati. Ndio maana nasema, ukishatokea kumpenda mtu na ukaamini kwamba naye ana mapenzi ya dhati kwako, usiyasikilize maneno ya watu.
Lazima iwe hivyo kwasababu, ukiwasikiliza kuna uwezekano mkubwa sana wa kukuyumbisha na hata kama moyo wako ulishaamua kumpenda huyo uliyenaye, utashangaa unaanza kupingana na moyo na kuhisi huenda kweli hukustahili kuwa naye.
Siku zote walimwengu hawakosi la kusema hivyo si wa kuwapa nafasi sana katika kufanya maamuzi yako hasa linapokuja suala la mapenzi. Si wote ambao watavutiwa na mpenzi uliyenaye, wengine watakwambia umedondoka sehemu ambayo siyo na washakunaku wanaweza kwenda mbele zaidi kumponda laaziz wako kuwa, ni kicheche na ameshatembea na watu kibao.
Ni suala la wewe kuwa na msimamo na kuamini katika kile ambacho umeamua. Umeamua kumpenda huyo uliyenaye, usiwape nafasi watu waanze kumjadili, waambie hata aweje, moyo wako ndiyo umetua kwake.

Post a Comment